maandamano ya bodaboda yakiendelea kumuunga mkono Bw.Ngalawa
huu ndio usafiri alioutumia Deo Ngalawa wakati akirudisha fomu ya ubunge
Deo Ngalawa akiwasalimia wananchi kwa kupunga mkono wakati akirudisha fomu ya ubunge
Cledo Filikunjombe ambaye ni mdogo wa hayati Deo Filikunjombe akiwa na gari yake akimuunga mkono Deo Ngalawa katika kuirudisha fomu ya ubunge wa jimbo la Ludewa.
Mgombea
ubunge wa jimbo la Ludewa kupitia chama cha mapinduzi Bw.Deo Ngalawa jana
alifunika wilaya ya Ludewa kwa kufanyiwa maandamano makubwa ambayo hayajawahi
kutokea wakati akirudisha fomu ya ubunge katika ofisi ya tume ya Taifa ya
uchaguzi wilayani hapa.
Akiongea na
wananchi mara baada ya kuikabidhi fomu hiyo kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la
Ludewa Bw.Ngalawa aliwaeleza wananchi kuwa hata waangusha katika uongozi wake kwani
atafuata nyayo za aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo hayati Deo Filikunjombe.
Bw.Ngalawa
alisema kuwa katika uongozi wake atafanya kazi zaidi katika sekta ya
elimu,Afya,Miundombinu na kukuza uchumi kwani bado wananchi wa wilaya ya Ludewa
wanahali ngumu kiuchumi hivyo imepelekea vijana wengi kukimbilia miji mingine
na kuhaimia huko.
“Sita
waangusha katika suala zima la maendeleo ni ukweli usiopingika kuwa hayati Filikunjombe aliyapeleka
maendeleo kwa kasi kubwa hivyo hata mimi nitafanya hivyo na nitajitahidi
kufanya kazi mara mbili yake ili wilaya ya Ludewa na wananchi wake wafurahie
matunda ya uhuru wa taifa letu”,alisema Ngalawa.
Alisema kuwa
maendeleo hayaletwi na mtu mmoja hivyo wananchi wanapaswa kushiriki ipasavyo
katika kuleta maendeleo na kujiletea maendele pia aliwataka vijana,akina mama
na wazee kuanzisha vikundi mbalimbali ambavyo vitaweza kukopesheka na kujiinua
kiuchumi.
Aidha katibu
wa chama cha mapinduzi wilaya ya Ludewa Bw.Lusiano Mbosa alisema kuwa katika
kata 26 jimbo la Ludewa CCM imeshinda
kata 25 na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimeshinda kata moja ya
Madope hivyo huo ni ushindi mkubwa kwa ccm ambao utaleta matokeo mazuri yasiyo
na shaka katika ubunge.
Bw.Mbosa
alisema mgombea wa ubunge kwa jimbo la Ludewa anauzika hivyo aliwataka wagombea
wengine ambao kura hazikutosha katika mchakato wa kura za maoni kumuunga mkono
Bw.Ngalawa katika kampeni zake ambazo zinatarajia kuanza hivi karibuni.
Akikabidhiwa
fomu za ubunge na mgombea wa ccm msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ludewa ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya hii Bw.William Waziri aliwataka wagombea kufanya kampeni za kistaarabu
ambazo zitajenga heshima kwa wananchi wa jimbo hili.
Bw.Waziri
alisema kuwa jimbo la uchaguzi la Ludewa lina wagombea wawili wa nafasi ya
ubunge ambao ni Deo Ngalawa kutoka chama cha mapinduzi na Bathromeo Mkinga(Msambichaka)
kutoka chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) hivyo kila mgombea
anapaswa kuwaeleza wafuasi wake kanuni
za uchaguzi ili amani iweze kutawala.
Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni