Jumatano, 2 Septemba 2015
Jumanne, 1 Septemba 2015
LIVE UPDATE Kutoka Serena Hotel Ambako Dr. Slaa Anaongea
2. Nimeamua kujitokeza leo hii ili kukomesha upotoshaji na kuuweka wazi ukweli.
3.Sina tabia ya kuyumbishwa na ninasimamia ninachokiamini.
4.Sina ugomvi na kiongozi yeyote maana siasa sio uadui.
5. Siasa inapoongozwa kwa misingi ya upotoshaji, matokeo yake ni vurugu.
6. Naweka wazi kuwa mimi sikuwa likizo na hakuna mtu yoyote aliyenipa likizo.
7.Kilichotokea
ni kuwa niliamua kuachana na siasa tangu tarehe 28.7.2015 saa
sita usiku baada ya kutoridhishwa na kilichokuwa kinaendelea
ndani ya chama changu.
Lowassa: Miaka 50 ya Kuteswa na CCM Imetosha......Watanzania Msiogope Kufanya Mabadiliko
Mgombea
urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amesema mwaka huu ni
wa mabadiliko ili kuiokoa nchi na madeni mengi ambayo yanasababisha
uchumi kuyumba.
Magufuli Atikisa Songea......Aweka shada la maua kwenye Kaburi la Marehemu Kapteni John Komba
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea jana ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi mkoani humo.
Akizungumza katika mkutano huo wakati akiomba kura Dr. John Pombe Magufuli aliwaambia wananchi hao kuwa anataka kuijenga Tanzania mpya yenye viwanda vikubwa, vya kati na vya chini ili kuboresha uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania na kuleta mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko.
Alisema
pia serikali yake itaongeza kasi ya ujenzi wa barabara , Zahanati na
Hospitali , kuongeza mafao ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali ili
kuongeza tija ya kazi , wanafunzi kusoma bure kuanzia darasa la kwanza
mpaka kidato cha nne nk.
Alisema
ataongeza zaidi kasi yake katika utendaji tofauti na
alipokuwa Waziri wa ujenzi kwani hapo awali alikuwa akiagizwa kama
waziri na sasa akichaguliwa na watanzania kuwa rais yeye ndiye
atakayeagiza na ole wake waziri atakayemteua asitekeleze maagizo yake
atakiona cha moto.
Dr
John Pombe Magufuli pia alitembelea na kuweka shada la maua kwenye
kaburi la Kada maarufu wa CCM marehemu Kapten John Damiano Komba ambaye
alifariki miezi kadhaa iliyopita jijini Dar es salaam katika hospitali
ya jeshi Lugalo na kuzikwa nyumbani kwao huko Lituhi wilaya ya Nyasa
mkoani Ruvuma
Mgombea
wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)