Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea jana ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi mkoani humo.
Akizungumza katika mkutano huo wakati akiomba kura Dr. John Pombe Magufuli aliwaambia wananchi hao kuwa anataka kuijenga Tanzania mpya yenye viwanda vikubwa, vya kati na vya chini ili kuboresha uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania na kuleta mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko.
Alisema
pia serikali yake itaongeza kasi ya ujenzi wa barabara , Zahanati na
Hospitali , kuongeza mafao ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali ili
kuongeza tija ya kazi , wanafunzi kusoma bure kuanzia darasa la kwanza
mpaka kidato cha nne nk.
Alisema
ataongeza zaidi kasi yake katika utendaji tofauti na
alipokuwa Waziri wa ujenzi kwani hapo awali alikuwa akiagizwa kama
waziri na sasa akichaguliwa na watanzania kuwa rais yeye ndiye
atakayeagiza na ole wake waziri atakayemteua asitekeleze maagizo yake
atakiona cha moto.
Dr
John Pombe Magufuli pia alitembelea na kuweka shada la maua kwenye
kaburi la Kada maarufu wa CCM marehemu Kapten John Damiano Komba ambaye
alifariki miezi kadhaa iliyopita jijini Dar es salaam katika hospitali
ya jeshi Lugalo na kuzikwa nyumbani kwao huko Lituhi wilaya ya Nyasa
mkoani Ruvuma
Mgombea
wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli akitoa heshima katika kaburi la Kada maarufu wa CCM Marehemu
John Damiano Komba katika kaburi lake huko Lituhi mkoani Ruvuma kulia ni
Mjumba wa Kamti kuu ya CCM Ndugu William Lukuvi.
Mgombea
wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Kapteni John
Komba huko Lituhi mkoani Ruvuma.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa kata ya Lituhi.
Umati
wa wananchi ukiwa umefurika katika uwanja wa taifa mjini Mbinga katika
mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Dr. John Pombe Magufuli.
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Mh William Lukuvi akiwapa salam za mikoa mingine ambako Dr. John Pombe Magufuli amepita.
Mgombea
wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli akihutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika
kwenye uwanja wa Taifa mjini Mbinga.
Umati uliohudhuria katika mkutano huo Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo uliofanyika Peramiho mkoani Ruvuma. Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiingia kwenye uwanja wa Majimaji.
Umati uliohudhuria katika mkutano huo Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo uliofanyika Peramiho mkoani Ruvuma. Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiingia kwenye uwanja wa Majimaji.
Majimaji ikiwa imetapika
Mwigulu Nchema akitema cheche kwenye uwanja wa majimaji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni