Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake ilifeli katika kutatua mzozo wa Libya.
Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake.
Bw
Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi taifa hilo
litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar
Gaddafi.
Alisema haya katika mahojiano na runinga ya Fox News kuangazia mafanikio na mapungufu ya utawala wake.
Hata
hivyo ametetea hatua ya kuingilia kijeshi nchini Libya. Marekani na
Muungano wa NATO zilitekeleza mashambulio ya anga kuwalinda raia baada
ya kuzuka maasi dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Lakini
baada ya mauaji ya kiongozi huyo, Libya ilitumbukia katika vita vya
wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi ya waasi huku makundi mawili
yakiunda serikali na mabunge tofauti.
Katika
hatua za kurejesha utulivu serikali ya muungano wa kitaifa inayoungwa
mkono na Umoja wa Mataifa imewasili katika mji mkuu Tripoli ili kuanza
mipango ya kuongoza nchi ya kurejesha hali ya kawaida.
Uchaguzi
mkuu nchini Marekani utafanyika Novemba na Rais Obama atakabidhi
madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani baada ya kuongoza kwa mihula
miwili.
Chanzo: BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni