Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
12 Aprili, 2016 ameungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki kuuaga mwili wa
Mbunge Mstaafu wa Mkoa wa Singida Marehemu Christina Lissu Mughwai
katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.
Christina Lissu Mughwai aliyekuwa Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Singida katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, alifariki dunia tarehe 07 Aprili, 2016 katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es salaam, alikokuwa akipatiwa Matibabu.
Pamoja na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Viongozi wengine waliohudhuria shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge Mheshimiwa Freeman Mbowe.
Akitoa salamu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa George Simbachawene amewapa pole familia ya marehemu na kueleza kuwa katika kipindi chake cha ubunge Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai alitoa mkubwa kama mbunge na kama mtaalamu wa Uchumi.
"Mheshimiwa Rais anatoa pole nyingine kwenu familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina" Amesema Mheshimiwa Simbachawene.
Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai umesafirishwa leo kwenda kijiji cha Mahambe Mkoani Singida kwa Mazishi.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
12 April, 2016

wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Mwanasheria
Tundu Lissu (Mb) kufatia kifo cha mdogo wake Christina Lissu Mughwai
aliyefariki Aprili 7 mwaka huu.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimpa pole Mwanasheria Tundu Lissu (Mb)
kufatia kifo cha mdogo wake Christina Lissu Mughwai aliyefariki Aprili 7
mwaka huu
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na
mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Freeman Mboye wakati wa akiaga mwili wa
marehemu Christina Lissu Mughwai aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum
kutoka Chadema katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli na mke wake mama Janeth
Magufuli wakiaga mwili wa marehemu Christina Lissu Mughwai aliyewahi
kuwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Chadema katika ukumbi wa Karimjee
jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni