Mgogoro wa uongozi ndani ya Chama cha Wanachi (CUF) unaendelea kuzua mapya ambapo jana, Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba alimvaa tena Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho
zilizoko Buguruni jijini Dar es Salaam, Profesa Lipumba alimtahadharisha Maalim Seif akimtaka aachane na ‘waganga’ kwani watamdanganya.
Ingawa
hakueleza ni waganga wa aina gani, Profesa Lipumba alimtaka Maalim Seif
kukubali kuzungumza naye ili wamalize matatizo yao.
“Haiwezi
kubadilika kwamba Mwenyekiti wa chama hiki nikiwa hai hadi mwaka 2019…
Maalim waganga watakudanganya sana, watakudanganya sana,” alisema
Profesa Lipumba.
“Katika
hili lilitakiwa lisifike hapa, huna sababu, njoo tuzungumze, pokea simu
yangu unajua namba yangu tuzungumze tuyamalize uje nikupangie kazi,”
aliongeza.
Mchumi
huyo alisisitiza kuwa hatakubali chama hicho kiuzwe kwa bei nafuu kwa
vyama vingine vya kisiasa au kwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya
Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward
Lowassa.
Kwa
upande wake Maalim Seif ameendelea kushikilia msimamo wake akieleza
kuwa Profesa Lipumba ni msaliti wa chama hicho na ana lengo la
kukivuruga.
Alisema
kuwa yeye yuko tayari kukaa naye meza moja kwa lengo la kueleza
hadharani kile alichokiita uongo wake na sababu halisi iliyomfanya
ajiuzulu nafasi ya Uenyekiti siku chache kabla ya kuanza kampeni za
uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni