Jumanne, 29 Novemba 2016

MWENYEKITI WA BODI YA SHIRIKA LA MAENDELEO LA TAIFA(NDC) APOKELEWA KWA MABANGO WILAYANI LUDEWA.


  Mabango wa wananchi wa Nkomang'ombe
  Mabango wa wananchi wa Nkomang'ombe

  Mabango wa wananchi wa Nkomang'ombe
Wananchi wa Mundindi katika mradi wa chuma wakiwa na mabango yao
 Wananchi wa Mundindi katika mradi wa chuma wakiwa na mabango yao
Mwenyekiti wa Bodi ya NDC Taifa Dr.Samwel Nyantahe mwenye shati nyeupe akiwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mh.Edward Haule katika maabara ya Makaa ya mawe Nkomang'ombe
Mwenyekiti wa bodi ya NDC Dr.Nyantahe akiwa na Viongozi mbalimabali katika mradi wa chuma Liganga
Dr.Nyantahe akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa MMI kuhusiana na uchimbaji wa chuma
Mwenyekiti wa bodi ya NDC Dr.Nyantahe akiwa na Viongozi mbalimabali wakiwemo maofisa kutoka ofisi ya mbunge wa jimbo la Ludewa katika mradi wa Makaa ya mawe Nchuchuma
Dr.Samwel Nyantahe akiongea na mwandishi wa mtandao huu Nickson Mahundi
Dr.Nyantahe akiwa na mwandishi na mmilikiwa mtandao huu Bw.Nickson Mahundi
Mwenyekiti wa bodi ya NDC Dr.Nyantahe akiwa na Viongozi mbalimabali katika mradi wa chuma Liganga

 Dr.Nyantahe akionesha jiwe la chuma kwa waandishi wa habari

Dr.Nyantahe akiwa na mwandishi na mmilikiwa mtandao huu Bw.Nickson Mahundi



Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Shirika la maendeleo la Taifa (NDC) Dr.Samuel Nyantahe amepokelewa kwa mabango yenye jumbe nzito wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kuashiria kukelwa na ahadi za Serikali ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na viongozi wa shirika hilo kuhusiana na ulipaji wa fidia katika maeneo yao.
Wakiongea kwa jazba jana wakati uongozi wa NDC ulipotembelea maeneo ya migodi ya Makaa ya mawe Nchuchuma na chuma cha Liganga katika kata ya Mundindi kwa lengo la kumuonesha Mwenyekiti huyo fulsa zilizopo maeneo hayo ili Serikali iendelee na utaratibu wa uwekezaji walisema kuwa wamechoshwa kuona viongozi wakifika maeneo hayo bila kutoa jibu la fidia ili kupisha uwekezaji italipwa lini.
Mmoja wa wananchi hao Bi.Angelina Mgeni mkazi wa kata ya Mundindi wilayani Ludewa alisema kuwa eneo ambalo zimejengwa kambi za wachina ambao ni wawekezaji wa miradi hiyo ndipo yalipokuwa makazi yao tokea akiwa mtoto mdogo lakini mpaka wazazi wake walifariki na kuzikwa eneo hilo alikuwa akisikia kutakuwa na uchimbaji wa chuma lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea.
Bi.Angelina alisema kuwa NDC waliwatoa eneo hilo ili kupisha wawekezaji na wakiahidiwa watalipwa fidia lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea hivyo ifikapo tarehe moja Januari 2017 kama hakuna malipo atarudi kupanda miti eneo lao la Familia bila kujari kuna nyumba za raia wakichina maana wameshindwa kufanya shughuri za kimaendeleo kwa muda mrefu na hivyo kuwafanya uchumi wao kudorola.
“nimezaliwa katika eneo hili na hata wazazi wangu wamezikwa katika mashamba haya ambayo kwa sasa ni kambi za wachina na baadae tukaamuliwa kuondoka eneo hili ili kupisha wawekezaji lakini tuliahidiwa kulipwa fidia ili tukatafute mashamba katika maeneo mengine na uthamini ulishafanyika na tukaelezwa tungelipwa tarehe moja julay mwaka huu lakini hakuna kinachoendelea,ikifika January mwaka ujao nitarudi kupanda miti katika eneo langu nimechoka kudanganywa”,alisema Bi.Angelina.
Wananchi hao walisema kuwa kijiji cha Mundindi kimekuwa nyuma kimaendeleo tofauti na vijiji vingine wilayani Ludewa kutokana na ahadi za shirika la maendeleo la Taifa (NDC)kuwazuia kuendeleza maeneo yao ili uwekezaji wa migodi hiyo uweze kufanyika lakini ahadi hizo zimekuwa hewa hali ambayo wananchi wanahitaji kurudishiwa Ardhi yao ili waendelee na uzalishaji mali.
Akijibu jumbe mbalimbali zilizoandikwa katika mabango zikiambatana na maswali mengi kutoka kwa wananchi Mwenyekiti wa bodi ya NDC Taifa Dr.Samwel Nyantahe alisema kuwa ni kweli wananchi ni haki yao kulalamika lakini wanatakiwa kuwa na subira kwani Serikali ya awamu ya tano ni ya viwanda hivyo yeye ni mwenyekiti mpya wa bodi hiyo na alifanya ziara hiyo ili kujiridhisha na uwepo wa utajiri huo.
Dr.Nyantahe alisema kuwa tayari fedha za ulipaji wa fidia zimeshatengwa na kilichokuwa kikifanyika ni kupitia upya mikataba hiyo na wawekezaji zoezi ambalo tayari limekwisha na hatua ya mwisho ni kupitishwa katika baraza la Mawaziri ili kubariki ulipaji huo uendelee hivyo wananchi wanatakiwa kupunguza jazba na kuiamini Serikali yao katika utekelezaji.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ambaye pia ni diwani wa kata ya Ibumi kupitia chama cha mapinduzi Mh.Edward Haule alimuomba mweyekiti huyo wa Bodi kuhakikisha majibu sahihi ya lini fidia inalipwa kwa wananchi hao kwani imekuwa ni kero kubwa kwa viongozi wa Serikali kutembelea katika kata hizo na kuongea na wananchi.
Mh.Haule alisema kuwa wananchi wa maeneo hayo walikuwa wakiitumia ardhi hiyo katika kujizalishia mali na kujipatia kipato ambacho kimekuwa ni msaada katika familia zao kama ulipaji wa ada za familia mashuleni lakini kwa kuzuiliwa kwa muda mrefu kutolima mazao ya kudumu katika maeneo hayo kumewarudisha nyuma katika maendeleo wakisubiri fidia ili wakanunue mashamba maeneo mengine.
Alisema kila viongozi wa ngazi ya wilaya wanapopanga ziara ya kuwatembelea wananchi hao mikutano huvurugika kutokana na hasira walizonazo wananchi hao katika kulipwa fidia zao hivyo kama kiongozi mkuu wa bodi ya NDC anapaswa kulitazama kwa umakini mkubwa jambo hilo ili kuleta amani baina ya viongozi wa kiserikali na wananchi hao katika kuleta maendeleo.
Mwisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa