Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati wa
Zambia, David Mabumba, wamekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuboresha
Bomba la Mafuta la TAZAMA ili liweze kuwanufaisha wananchi wa Tanzania
na Zambia kama ilivyokusudiwa.
Mazungumzo
yao yaliyofanyika mapema leo, ofisini kwa Waziri Muhongo jijini Dar es
Salaam, ni kufuatia makubaliano ya marais wa nchi husika, Dk John
Magufuli na Edgar Lungu; kuhusu kuboresha zaidi Bomba la TAZAMA na Reli
ya TAZARA.
Marais
Magufuli na Lungu, walifikia makubaliano hayo jana katika mazungumzo
rasmi yaliyofanyika Ikulu ya Dar es Salaam ambayo ni mojawapo ya
shughuli mbalimbali zilizopangwa katika ratiba ya ziara ya siku Tatu (3)
ya Rais Lungu iliyoanza nchini Jumapili, Novemba 21 mwaka huu.
Waziri
Mabumba ambaye alifuatana na Ujumbe wa Viongozi na Maafisa waandamizi
kutoka TAZAMA na wizarani kwake; aliafiki mapendekezo yaliyotolewa na
Waziri Muhongo kuhusu namna pande hizo mbili zitakavyoshirikiana katika
utekelezaji wa agizo la Marais wao ambayo ni pamoja na wataalam wa pande
zote kukutana na kufanya majadiliano pamoja na kufanya ziara kukagua
utendaji kazi wa Bomba hilo.
Aidha, Mawaziri hao walijadiliana kuhusu namna ambavyo Zambia itanufaika na gesi asilia iliyogunduliwa Kusini mwa Tanzania.
Kikao
hicho pia, kilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Wizara ya Nishati na
Madini – Tanzania, akiwamo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa James
Mdoe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni