Jeshi
la Polisi limewakamata watu 38 wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi ambao
pia wamepatiwa mafunzo ya kigaidi katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani
na Lindi.
Sambamba na kukamatwa watu hao, polisi pia imekamata bunduki 10, risasi 300 na bomu moja la mkono.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna, Suleiman Kova
ametangaza leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam.
Kova aliongeza kuwa watuhumiwa hao pia wanajihusisha na kutoa mafunzo ya kigaidi.
‘’
Hawa tumefanikiwa kuwakamata, tunawaita majambazi au magaidi kwa kuwa
licha ya kufanya ujambazi pia wanajihusisha na kutoa mafunzo ya kigaidi
katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Lindi,’’ alisema Kamanda Kova.
Amesema
kuwa polisi wamefanikiwa kuwanasa watu hao ikiwa ni operesheni endelevu
ya kuwasaka wahalifu wote wanaovunja amani hapa nchini.
Ameeleza
kuwa baadhi ya silaha zilikamatwa zikiwa zimefichwa maeneo ya Mkuranga
mkoani Pwani ambapo baadhi ya silaha hizo tayari zilikuwa zimeshapata
kutu.
Kamanda
Kova amesisitiza kuwa polisi wanaendelea na upelelezi na ukishakamilika
watuhumiwa hao watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na
kufikishwa mahakamani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni