
Mkutano Mkuu wa CHADEMA ulianza kwa kuimba nyimbo ya taifa

Shehe Rajabu Katimba akiomba Dua wakati wa mkutano mkuu wa CHADEMA uliofanyika leo

Mchungaji Zakaria Kakobe akitoa neno la mungu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

Naibu katibu Mkuu Zanzibar Mh. Salum Mwalim akifungua mkutano wa Baraza kuu uliofanyika leo

Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mh. Freeman Mbowe akisoma
hutuba katika mkutano mkuu wakati wa mkutano mkuu uliofanyika leo kwenye
ukumbi wa mlimani City jijini Dar

Makamu
wa kwanza wa Urais Zanzibar Mh Maalimu Seifu akizungumza jambo ambapo
alisema " Kwa uwezo wa Mwenyezi mungu tutaweza kuingoa CCM kwani
watanzania wako tayari kuyafata mabadiliko.na pia Mpaka dakika hii
sijapata barua ya Prof Ibrahim Lipumba kujiuzulu na mpaka jana saa 4
usiku nilikuwa nae na sikuona dalili zozote za kuonyesha kupishana na
jambo hili kama jinsi ilivyoripotiwa na moja ya gazeti.

Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi taifa ,James Mbatia wakati anazungumza aliwauliza wajumbe
wa mkutano huo kwamba mbona Mkutano Mkuu huu hauna magari ya washawasha
na mabomu, Hii ni dhahiri kuonyesha kuwa imani imetawala ndani ya
Chadema pamoja na UKAWA kuelekea safari ya uchaguzi Mkuu.

Mwenyekiti
wa waalimu Mh. Graison Graison Mkoba wakati wa anazungumza kwenye
mkutano mkuu wa chadema alisema " Niliambiwa na rafiki yangu mmoja afisa
misitu kuwa ukiukata mti usiuzuei awache uporomokea kuelekea unapotaka
hata kama unataka kupasua mbao ukiuzuia utakufa"Na " Unapochemsha maji
ili kumkimbiza chura itachukuwa muda chura kukimbia mpaka joto lipande
kwenye maji ndio chura aondoke" hayo ndio maneno ninayowaachia wajumbe
wa Mkutano Mkuu CHADEMA

Juma
Duni Haji mgombea mwenza wa UKAWA kupitia CUF wakati anazungumza kwenye
mkutano huo alisema "Nimechukua maamuzi magumu kama Mh Edward Lowassa
ili Kuimarisha UKAWA."Mimi nimeanza siasa nikiwa form 2 mambo nilikuwa
na afro shirazi party mambo yalivyobadilika na mm nikabadilika napata
kustaajabu ninapomuona askari aliyotoka katika familia ya kimaskini
anakabidhiwa silaha kuwalinda wananchi na badala yake anapiga mtoto wa
kimaskini dhana ya kutafuta uhuru imepotea"

Mgombea
wa Urais alieteuliwa na chama hicho, Mh. Edward Lowassa akiwashukuru
wananchama wa CHADEMA kwa kumpokea na kuonyesha upendo wao na kuwaahidi
kuwa atayakabili majukumu makubwa waliyomkabidhi.

Pia
wakati anazungumza alisema "Niwaahidi kuwa tutafanya kampeni za
kiistarabu sio kampeni za matusi na tutashinda kwa kishindo
kikubwa. Niwaahidi watanzania kuwatumikia kwa hali namali na wategemee
mabadiliko makubwa."

Mgombea
wa Urais alieteuliwa na chama hicho, Mh. Edward Lowassa akiwa kwenye
picha ya pamoja na Mgombea Mwenza wake, Mh. Dkt. Juma Haji Duni

Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (wa
pili kushoto) akiwa ameshikana mikono na Mgombea wa Urais alieteuliwa na
chama hicho, Mh. Edward Lowassa (wa kwanza kushoto) pamoja na Mgombea
Mwenza wake, Mh. Dkt. Juma Haji Duni (wa pili kutoka kulia) pamoja
na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
(kulia), wakati wakitambulishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama hicho,
uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es
Salaam.

Picha
ya pamoja ya wenyeviti, wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wanachi
(UKAWA) Makamu wenyeviti na Naibu Makatibu wakuuwa wa Cahadema wakiwa
na mgombea urais Edward Lowassa na mgombea mwenza Haji Duni kwenye picha
ya pamoja

Wananchama wakiwa ndani ya mkutano


Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni