Jumatatu, 31 Agosti 2015

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI JESHI LA POLISI

TANGAZO KWA UMMA.

JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAITA KWENYE USAILI WAHITIMU WALIOORODHESHWA WA SHAHADA, STASHAHADA NA ASTASHAHADA. USAILI UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 03.09.2015 HADI TAREHE 04.09.2015 KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI HADI SAA KUMI JIONI KATIKA MAENEO YAFUATAYO:-
·         FANI YA UTAWALA, UCHUMI, USIMAMIZI WA SHERIA NA UTEKELEZAJI [BALE], UALIMU, UANDISHI HABARI, UHANDISI MADINI [MINING ENGINEERING], UGAVI, LUGHA, USHAURI NASIHI, KATIBU MUKTASI, LAND SURVEY CATHOGRAPHER NA GEOMATICS WATAFANYA USAILI KATIKA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR ES SALAAM [DPA] KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM.
·         MAFUNDI MAGARI, MATENGENEZO YA PIKIPIKI, MAFUNDI MATENGENEZO YA UMEME WA MAGARI [AUTO ELECTRICAL], MAFUNDI RANGI ZA MAGARI, MAFUNDI MAGARI, MAFUNDI USHONAJI,MAFUNDI BODY ZA MAGARI NA MADEREVA. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI UFUNDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
·         MATENGENEZO YA KOMPYUTA, FAX & PHOTOCOPY MACHINES NA MAWASILIANO YA REDIO [DIPLOMA IN RADIO COMMUNICATION], USAILI WAO UTAFANYIKA NYUMA YA KIKOSI CHA UFUNDI YAANI TEHAMA KEKO CHINI.
·         WAKEMIA, BAILOJIA [MOLECULAR BIOLOGY] USAILI UTAFANYIKA MAKAO MAKUU YA POLISI YALIYOPO MAKUTANO YA BARABARA YA OHIO NA GHANA JENGO LINALOTAZAMANA NA POSTA HOUSE.
·         KADA ZA AFYA USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA AFYA KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
·         MANAHODHA NA MAFUNDI MITAMBO WA MELI, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA WANAMAJI KILICHOPO KARIBU NA JENGO LA MAHAKAMA YA RUFAA.
·         DAKTARI WA WANYAMA, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA MBWA NA FARASI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
·         MAFUNDI AC ZA MAJUMBANI, ARCHITECTURE DRAFTMAN, QUANTITY SURVEYORS, CIVIL ENGINEER, WELDING & FABRICATION, UMEME WA MAJUMBANI, PAINTING, ALUMINIUM & GLASS WORK, PLUMBING, MOSONRY, MOTOR REWINDING, HYDRO GEOLOGY DRILLING WELL, REFRIGERATION & AIR CONDITIONING. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI UJENZI NDANI YA KAMBI YA POLISI BARRACKS KURASINI KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
·         FANI ZA BENDI, BRASS BENDI, WOODWIND, STRING JAZZ NA PERCUSSIVE, USAILI WAO UTAFANYIKA KIKOSI CHA BENDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
·         FANI YA URUBANI,USAILI  UTAFANYIKA  KIKOSI CHA ANGA KILICHOPO UWANJA WA NDEGE NDOGO WA ZAMANI WA J.K.NYERERE DSM.

MUHIMU:
1.      MWOMBAJI AFIKE KWENYE USAILI AKIWA NA NAKALA HALISI YA VYETI VYOTE VYA MASOMO/TAALUMA [ACADEMIC TRANSCRIPT (S)/CERTIFICATE (S) YAANI KIDATO CHA NNE, SITA, CHUO NA CHETI CHA KUZALIWA. KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIWA.
2.      MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI ATALIPIA GHARAMA ZA UPIMAJI AFYA SHILINGI ELFU KUMI (10,000/=), USAFIRI, CHAKULA NA MALAZI KWA MUDA WOTE WA ZOEZI LA USAILI.
3.      AMBAYE HATAHUDHURIA USAILI KUANZIA SIKU YA KWANZA HATAPOKELEWA.
ILI KUPATA/KUONA ORODHA YA MAJINA, TEMBELEA www.policeforce.go.tz
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa