Jumatano, 9 Desemba 2015

Rais Magufuli Awaongoza Watanzania Kufanya Usafi

Rais John Magufuli ameongoza kwa vitendo zoezi la kufanya usafi leo kama alivyoelekeza baada ya kufuta shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Uhuru, Disemba 9.

Rais Magufuli na mkewe Janeth wamefanya usafi katika maeneo ya Feri, eneo ambalo liko mita kadhaa kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam.

Naye rais wa serikali ya awamu ya nne, Jakaya Kikwete na mkewe Salma nao wameingia barabarani na kuungana na wananchi kufanya usafi katika maeneo yao katika harakati za kutokomeza magojwa yanayotokana na uchafu kama kipindupindu.

Aidha, Makamo wa rais, Samia Suluhu yeye ameonekana akifanya usafi katika eneo la ufukwe wa bahari wa ‘Coco Beach’ jijini Dar es Salaam huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa yeye ameingia katika eneo la Soko la Kariakoo kujiunga na zoezi hilo.

Wananchi kwa ujumla nchini wameonekana kuitikia wito wa kufanya usafi katika maeneo yao kwa hamasa kubwa hali inayoonesha kuwa Tanzania itaweza kutokomeza magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uchafu.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa