Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limefanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Mkoani hapa pamoja na Kusafisha kambi zao kwa lengo la kuadhimisha miaka 54 ya uhuru na kutekeleza agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufanya usafi sikukuu hiyo.Pichani ni askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa wamebeba vifaa vya usafi kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo mbalimbali yanayozunguka kambi ya jeshi hilo-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Tunakwenda kufanya usafi....Hapa Kazi tu.....
Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Justus Kamugisha akiwa nje ya ofisi yake wakati askari polisi mkoa wa Shinyanha wakielekea kufanya usafi...Akizungumza na Malunde1 blog Kamanda Kamugisha amesema jukumu la kufanya usafi wa mazingira ni la kila mtu hivyo na wao wameamua kuadhimisha kufanya usafi huo kwa kuunga mkono agizo la Rais John Magufuli katika kuadhimisha siku ya Uhuru.
Tunakwenda kufanya usafi
Kamanda Kamugisha akitoa maelekezo kwa askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga..Kamugisha aliiambia Malunde1 blog kuwa magonjwa yatokanayo na uchafu hayabagui wadhifa wa mtu, bali yakitokea yanamkuta yeyote yule ,hivyo jeshi hilo limeamua kufanya usafi huo wa mazingira katika maeneo yao pia, ili kujikinga na magonjwa hayo ya mlipuko yasiweze kuwapata askari na kushindwa kulinda usalama wa raia na mali zao
Askari polisi mkoa wa Shinyanga wakifanya usafi katika maeneo yanayozunguka kambi yao mjini Shinyanga
Usafi unaendelea
Usafi unaendelea
Askari polisi wakifanya usafi katika eneo la Round About karibu na ofisi yao
Usafi unaendelea
Tunafanya usafi.....
Usafi unaendelea
Tunafanya usafi...
Askari wakiendelea kufanya usafi
Usafi unaendelea...
Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni