WIZARA
ya Nishati na Madini imeikanusha habari iliyotolewa kwenye gazeti la
Mtanzania la tarehe 14 Januari 2016 kichwa chake cha habari
kilichosomeka “HARUFU YA JIPU MRADI WA UMEME” aliyoandika mwandishi wa
gazeti hilo Jonas.
Habari
hiyo ilieleza kuwa, mradi uliozinduliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya
nne, Mh Jakaya Mrisho Kikwete uligharimu shilingi Trilioni 1.6 na kwamba
fedha za ujenzi wa mradi huo zimetokana na ubia kati ya serikali ya
Tanzania na Japan ambapo serikali ya Tanzania itakuwa na hisa ya
asilimia 40 na kampuni ya SUMITOMO ya Japan asilimia 60,pia taarifa hizo
zilidai kuwa serikali inachangia fedha za ndani kwa asilimia 12na
zilizobaki ni mkopo kutoka benki ya Japan.
Mwandishi
wa gazeti la Mtanzania alidai kuwa gharama za mradi huo ni kubwa
ukilinganishwa na miradi mingine akitolea mfano wa kampuni ya TALLAWARA
Power Station ya nchini Australia anayodai ilitaka kujenga mradi huo kwa
dola za kimarekani milioni 350.
Kwa
mujibu wa habari hiyo, Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra
Masoud ametolea ufafanuzi wa habari hiyo na kudai kuwa si ya kweli.
“Tunakanusha
vikali taarifa hizi zilizotolewa na kwamba hazina ukweli wowote
zimelenga kupotosha ukweli na kuichafua serikali.”Alisema Badra wakati
akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam
Badra
alifafanua ukweli wa mradi huo na kudai kuwa serikali ya Tanzania
iliingia makubaliano na Serikali ya Japan ya mkopo wa masharti nafuu wa
dola za kimarekani milioni 292 kwa aajili ya kutekeleza Mradi wa
kuzalisha umeme wa Megawati 240 utakaojengwa na kampuni ya SUMITOMO ya
Japan kama mkandarasi EPC contractor na sio kama mbia na serikali ya
Tanzania kama ilivyodaiwa.
“Mradi
unamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 kupitia TANESCO na hakuna
mwekezaji mwingine katika mradi huo,hivyo si kweli kwamba serikali ya
Tanzania imewekeza kwa ubia wa asilimia 40 na kampuni ya SUMITOMO kwa
silimia 60.Kwa maana hiyo hatutauziwa umeme utakaozalishwa na mradi huu
kwani ni mali yetu.”Aliongeza Badra
Pia alisema kuwa mradi wa Kinyerezi 2 bado haufunguliwa kama habari hiyo ilivyodai,mradi uliofunguliwa ni wa Kinyerezi 1.
Badra
alimaliza kwa kuwataka Waandishi wa Habari kufuata miiko na maadili ya
uandishi wa Habari kwa kuandika habari zenye ukweli na sahihi badala ya
kuandika habari za mitaani kwakuwa zinapotosha jamii
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni