Ajali
Mbaya imetokea leo asubuhi eneo la Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam
ikihusisha malori mawili na daladala iliyo kuwa ikitokea Gongo la Mboto
kuelekea Ubungo
Kwa mujibu wa mganga mkuu Hospitali ya Amana, Dr Stanley Binagi, watu wanne wamefariki dunia huku 25 wakijeruhiwa.
Inaelezwa kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma, hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugongana na Lori lingine lililokuwa limepakia Ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu Mnadani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni