Ijumaa, 4 Machi 2016

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AONGOZA MAANDAMANO YA MAOMBI YA AKINA MAMA LUDEWA

 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Rehema Nchimbi akiwa na akina mama wakati wa maandamano hayo leo.



 Akina Mama na watu wengine wengi wakiwa katika maandamano kuelekea Kanisa la Rc Ludewa Mjini.
Bodaboda nao hawakuwa mbali katika kuhakikisha msafara unakuwa mzuri.




Akina mama hawa na watu wengine wakifika Kanisa la Rc Ludewa Mjini ambako maombi yalifanyika.

 Hii ndio kauli mbiu/Neno kuu la Maombi hayo.

 Mkuu wa Wilaya ya Ludewa pamoja na Wachungaji wakishangilia na kufurahia maandamano hayo.


Na, Azaria Hule Ludewa.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Rehema Nchimbi leo ameongoza mamia ya akina mama katika siku ya maombi ya Dunia nzima yaliyofanyika katika kanisa na Roman Catholiki Ludewa Mjini. Maombi hayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuiombea Nchi ya Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla.

Maombi hayo yanajumuisha muungano wa Makanisa matatu ambayo ni Anglikana, Lutheran na Roman Catholic, ambapo umoja huo umeanza rasmi kwa kuunda uongozi wa akina mama hao mwaka 2015, wakati kwa miaka mitatu ya nyuma umoja huo ulikuwa ni wa Anglikana na Lutheran pekee.

Aidha katika Maombi hayo Mgeni Rasmi alikuwa ni Mh. Mbunge wa Jimbo la Ludewa Deo Ngalawa lakini hakufanikiwa kushiriki kutokana na Safari ya kikazi, hata hivyo badala yake aliyemwakilisha alikuwa ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mh. Edward Haule Diwani wa Kata ya Ibumi.

Katoka Hotuba ya Mgeni Rasmi, Mh. Mbunge Deo Ngalawa alikubali kuwasaidia akina mama hao Mashine ya kutotolesha vifaranga vya kuku kama mradi wako kutokana na malengo waliyojiwekea katika kuleta maendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla.

Pia katika kuunga mkono harakati za Akina mama hao Mkuu wa Mkoa wa Njombe Rehema Nchimbi alitoa Taslimu kiasi cha Tsh 1,100,000/= kama sadaka yake ili kuunga mkono jitihada za akina mama hao na pia aliwatia moyo sana katika kuleta maendeleo na kuiombea nchi ya Tanzania Mkoa na Wilaya ya Ludewa. Pia aliwaasa akina mama hao kuandaa mipango na mikakati ya kujitegemea na si kusubiri misaada ambayo wakati mwingine haiwezi kuwa na mafanikio yoyote.

MWISHO.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa