Jumatatu, 14 Machi 2016

Putin aagiza jeshi lake kuondoka Syria


Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa amri kwa wanajeshi walioko Syria kurejea nyumbani mara moja kwa sababu tayari wametekeleza asilimia kubwa ya malengo yao.

Akizungumza katika ikulu ya Kremlin Putin, alisema
''Tayari tumeshakamilisha asilimia kubwa ya madhumuni yetu nchini Syria kwa hivyo kuanzia jumanne (kesho) ningependa asilimia kubwa ya jeshi letu kurejea nyumbani.'' alisema bwana Putin.
Tangazo hilo lake limewaacha wachanganuzi wengi wamepigwa na mshangao kwani hakukuwa na dalili zozote za kuwepo kwa tukio kama hilo.
Aidha Putin ametangaza hilo katika siku ambayo mazungumzo ya amani yameanza upya mjini Geneva Uswisi.
Urusi ni mshirika wa karibu sana wa rais wa Syria Bashar al-Assad.
Image caption Urusi ni mshirika wa karibu sana wa rais wa Syria Bashar al-Assad.
Ikulu ya Kremlin inasema kuwa rais Bashar al-Assad alifahamishwa kuhusu hatua hiyo.
Itakumbukwa kuwa kuingia kwa majeshi ya Urusi katika vita vya Syria vilibadili kabisa taswira ya vita hivyo.
Kwa wakati huo waasi walionekana kuwa walikuwa wanaelekea kuishinda nguvu jeshi la Syria kinyume na hali ilivyo sasa ambapo majeshi watiifu kwa rais Assad wameanza hata kuteka maeneo yaliyokuwa chini ya waasi.
Rais Putin hata hivyo amesema kuwa kambi ya kijeshi ya Hmeimim na bandari ya Tartus itasalia chini ya jeshi la Urusi.
Huku akisisitiza kuwa zitalindwa ''kwa hewa ardhini na hata baharini''

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa