Jumatatu, 14 Machi 2016

Walimu Wanaotuhumiwa Kufanya Mapenzi na Wanafunzi Jijini Mwanza Waundiwa Kamati Maalum


Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Mwanza kimeunda kamati kuchunguza tuhuma dhidi ya baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari Mihama wilayani Ilemala kujamiiana na wanafunzi wao.

Mwenyekiti wa CWT mkoani hapa, Sibora Kisheri alisema wameunda kamati hiyo baada walimu wanane, akiwamo mkuu, Joseph Marifedha kusimamishwa kazi kwa amri ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo, Magessa Mulongo kwa tuhuma hizo.

“Haiingii akili kuona walimu wote wakawa na sifa ya makosa yanayofanana, hivi hakuwapo hata mmoja aliyeshtukia mchezo huo na kuwashauri wezake,” alisema Kisheri.

Alisema uchunguzi huo unalenga kubaini kiini cha tuhuma hizo na kuishauri Serikali na vyombo husika hatua stahiki za kuchukua kuhakikisha kila upande unatendewa haki.

Aliwaasa walimu kufuata sheria, kanuni na misingi ya kazi kwa kutimiza wajibu na kuepuka mambo yanayokinzana na taaluma hiyo.

Hivi karibuni Mulongo aliwasimamisha walimu hao baada ya kupata taarifa kuwa walikuwa wakijihusisha na vitendo hivyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa