Jumatano, 9 Desemba 2015

TAZAMA PICHA ZA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA KUFANYA USAFI LEO KATIKA MKOA WA ARUSHA







Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limefanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Mkoani hapa pamoja na Kusafisha kambi zao kwa lengo la kuadhimisha miaka 54 ya uhuru na kutekeleza agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufanya usafi sikukuu hiyo.Pichani ni askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa wamebeba vifaa vya usafi kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo mbalimbali yanayozunguka kambi ya jeshi hilo-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog


Tunakwenda kufanya usafi....Hapa Kazi tu.....

Rais Wa Zanzibar Dk Shein Ashiriki Shughuli za Usafi Kuadhimisha Siku ya Uhuru.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Zanzibar Khatib Abrahman Khatib wakati alipowasilikati eneo la Malindi Mjini Zanzibar katika zoezi ka Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililoshirikisha Viongozi na Wananchi mbali mbali nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizoa taka katika  zoezi ka Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka 54 ya

Rais Magufuli Awaongoza Watanzania Kufanya Usafi

Rais John Magufuli ameongoza kwa vitendo zoezi la kufanya usafi leo kama alivyoelekeza baada ya kufuta shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Uhuru, Disemba 9.

Rais Magufuli Atoa Namba yake Ya Simu Kwa Wavuvi.....Awaahidi Mambo Matatu.

Rais John Magufuli leo ameungana na wananchi katika kufanya usafi ambapo akiwa katika eneo la Feri jijini Dar es Salaam, ameweza kuzungumza moja kwa moja na wavuvi wadogo.

Picha 3 za Waziri Mkuu Akishirikiana na Wananchi Kufanya Usafi Kariakoo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015. 

Alhamisi, 3 Desemba 2015

Magufuli: Sijachangiwa na Mfanyabiashara Yeyote Kuingia Ikulu.


Rais Dk. John Magufuli, amesema hakuna mfanyabiashara aliyemchangia  kumuwezesha kuingia Ikulu katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, ili aweze kusimamia ipasavyo makusanyo ya kodi kwa faida ya wananchi.

Jumanne, 1 Desemba 2015

Sad News: Basi la Takbir Lagongana na Lori Usiku Huu na Kuua Watu Kadhaa


Habari zilizotufikia usiku huu zinaarifu kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha katika ajali mbaya iliyotokea baada ya basi la abiria la Takbir lenye namba za usajili T 230 BRJ lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana na lori eneo la Shelui, kijiji cha Kizonzo omkoani Singida.

MREMA ASEMA HAJUTII KUMNADI RAIS MAGUFULI


MWENYEKITI wa Taifa wa chama cha siasa cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema amesema hakufanya makosa na wala hajutii kumnadi Rais John Magufuli kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa sababu alitambua Watanzania wamelamba dume la maendeleo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano Ya Disemba 2

Jumla ya Mara Iliyotazamwa