Kamati kuu maalum ya chama cha mapinduzi Zanzibar kwa kauli moja
imempitisha Dr Ali Mohamed Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia
chama cha mapinduzi.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya wajumbe wa NEC wa Zanzibar wanounda
kamati maalum ya Zanzibar kukutana hapa Zanzibar katika ofisi kuu ya CCM
na kuamua kumuidhinisha Dr Shein kugombea tena kiti hicho cha urais
baada ya wajumbe karibu 102 ambao ni aslimia 83 kuridhia Dr Shein
agombee.
Awali Dr Shein ambaye ni makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar
alilazimika kuondoka ndani ya kikao ili ijadaliwe na wanachama hao
ambapo kiti hicho kilishikwa kwa muda na Dr Mohamed Gahribu Bilali makamu
wa rais, ambapo baadaye akizumgumza na wanaccm hao waliokubali Dr Shein
aliwahidi wanachama wa CCM kuwa uamuzi wake uko palepale wa kutekeleza
ilani ya CCM ya kuitumikia Zanzibar.
Katika hatua nyengine naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar akizungumza
baada ya kikao hicho alisema CCM haiwezi kupinga au kukubali suala la
majimbo,wao wanasubiri maamuzi ya tume na wako tayari kwa umauzi wowote
utakaotolewa na tume ya uchaguzi ambayo inatarajiwa kutangaza majimbo
mapya leo asubuhi.
Kupitishwa kwa Dr Shein kugombea urais wa Zanzibar na kamati maalum
ni hatua ya kwanza na sasa shuguhli yote inahamia Dodoma ambapo jina la
Dr Shein litajadiliwa na kamati kuu na baadaye kutakiwa kuidhinishwa na
kupitishwa na halmashuri kuu ya CCM, nafasi ya urais wa Zanzibar
inaamuliwa na NEC na siyo na mkutano mkuu waccm.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni