Mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina la Ester Banzi, mkazi wa Tabata Msimbazi, jijini Dar es Salaam, ametekwa na kubakwa hadi kupoteza maisha baada ya mtu asiyefahamika kufanya kitendo hicho na kutokomea sehemu isyojulikana.
Inadaiwa kuwa siku ya tukio mtoto huyo alikutwa amefariki baada ya
kuingiliwa kimwili na mwanaume ambaye inadaiwa kuwa alimteka kwanza
kabla ya kufanya kitendo.
Kwa mujibu mama mdogo wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la
Watende Hamis, amesema kuwa siku ya tukio mama wa marehemu (Rebeka)
alimtuma Ester, dukani kununua unga na kudai kuwa sio mara ya kwanza
kwa mtoto huyo kutumwa dukani.
Inadaiwa kuwa muda ulizidi kwenda bila mtoto huyo kurudi kwani duka
halikuwa mbali na nyumbani, ikabidi wamfuatilie kwa watoto wengine ambao
huwa akicheza nao lakini hawakumpata na watoto hao walidai kuwa
walimuona na mfuko wa rambo akiwa ameongozana na baba mmoja.
Amedai kuwa waliendelea na juhudi za kumtafuta na kumtaarifu baba
mzazi wa mtoto huyo ambaye alienda kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi
Tabata Shule, na kudai kuwa ndani ya masaa matatu baba wa mtoto huyo
aliwapigia simu kuwa mtoto ameokotwa huku mwili ukionesha kuwa alibakwa
na kuharibiwa vibaya.
Kwa mujibu wa majirani wamedai kuwa walisikia sauti ya mtoto akiomba
msaada na ndipo wakaangalia eneo hilo na kumuona mtoto huyo na baada ya
kumchunguza wakagundua kuwa amebakwa kwani nguo yake ya ndani ilikuwa
pembeni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni