Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuri mara baada ya kuteuliwa kuipeperusha Bendera ya Chama cha Mapinduzi(CCM) katika uchaguzi mkuu ujao amemteua Samia Suluhu Hassan kuwa makamu wake wa Rais endapo atashinda katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza kwa furaha katika ukumbi mpya wa CCM uliopo hapa mkoani
Dodoma Magufuli amesema alipoteuliwa kuwa Naibu waziri Samia alikuwa
ndiye waziri wake hivyo yeye ndiye aliyemfundidha kufanya kazi na kupata
ujasiri uliomfikisha hadi sasa anateuliwa kushika wadhfa mkubwa ndani
ya chama cha Mapinduzi.
Magufuri amewashukuru wajumbe kwa uteuzi huo na kuwa
na imani naye huku akiwaahidi kuwa anaenda kutenda yale yote waliyo
mtuma na kuahidi kuitekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka
2015-2020.
Ushindi huo wa Magufuli umepokelewa kwa shangwe na wanasiasa
takribani wa kambi zote zilizokuwa zinasigana na kutishia kuleta
mtifuano ikiwemo baadhi ya wajumbe kutangaza kutokubaliana na maamuzi
ya chama kwa uteuzi huo akiwemo Mbunge wa Songea Emmanuel Nchimbi.
Kwa upande wa wajumbe wanawake kutoka maeneo mbalimbali wamesema kuwa
wana imani na Magufuli kwa kuwa ni mtu wa vitendo na sio wa maneno kama
walivyo wanansiasa wengine.
Magufuli alichukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa ndani ya chama
cha mapinduzi tarehe nne juni na kuacha gumzo kwa waandishi wa habari
kufuatia kuwakacha Waandishi waliokuwa wana msubiri pamoja na wanachama wa
chama cha Mapinduzi waliokuwa ukumbini wakimsubiri azungumzie
vipaumbele vyake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni