Wanasiasa wa upinzani nchini wamepinga kitendo cha mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kutumia ndege ya Serikali kwenye shughuli za kichama za kujitambulisha wakisema hatua hiyo ni matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa.
Dk Magufuli, juzi alikwenda Mwanza
kwa ziara maalumu ya kujitambulisha akitumia ndege ya Serikali aina ya
Fokker F28, jambo ambalo limeibua hisia tofauti.
Hata
hivyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA),
Kapteni Keenan Mhaiki alisema kitendo cha CCM kutumia ndege ya Serikali
hakivunji sheria na taratibu zozote kwa kuwa mbali na kusafirisha
viongozi wa Serikali, pia wanaruhusiwa kufanya biashara kwa kuhudumia
umma.
Pia, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye alisema walifuata taratibu zote kuikodi ndege hiyo na kwamba
chama chake ni kikubwa na hakiwezi kushindwa kukodi usafiri huo.
“Ile
ni ndege ya Serikali, yeyote anayetaka kuitumia aende kulipia tu,
atapewa. Sisi tumekwenda kama wateja wa kawaida tukalipia, ukitaka kujua
ni kiasi gani kawaulize wahusika watakueleza,” alisema Nape.
Kuhusu
suala hilo la gharama, Kapteni Mhaiki alisema gharama ya kukodi ndege
hizo zipo tofauti kutokana na aina inayohitajika akisema aliyoitumia Dk
Magufuli inagharimu Dola za Marekani 4,000 sawa na Sh8.4milioni kwa saa
moja.
Akizungumzia suala hilo jana, Kiongozi wa chama
cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe alisema viongozi wa Serikali wamekuwa
na utamaduni wa kutumia mali za umma kwa shughuli za kisiasa na kusahau
kwamba rasilimali hizo ni za Watanzania wote bila kujali itikadi zao.
Zitto na Mbowe
Zitto
alisema jambo hilo halijaanzia kwenye ziara ya Dk Magufuli, bali hata
mawaziri wote waliochukua fomu walitumia magari ya Serikali kuzunguka
nchi nzima kutafuta wadhamini wao kwa nafasi ya urais.
“Jambo
hili si kwa CCM pekee, tunaona pia gari la Kiongozi wa Upinzani Bungeni
(KUB), likitumika kwenye mikutano yake ya kichama. Lile ni gari la
Serikali; kwa hiyo lazima tuupige vita utamaduni huu,” alisema Zitto.
Alisema CCM ina wajibu wa kuwaeleza Watanzania sababu za kutumia ndege ya Serikali na kama wamelipia fedha ni kiasi gani kilicholipwa huku akisisitiza kuwa utamaduni huu uliokithiri unaligharimu Taifa.
Alisema CCM ina wajibu wa kuwaeleza Watanzania sababu za kutumia ndege ya Serikali na kama wamelipia fedha ni kiasi gani kilicholipwa huku akisisitiza kuwa utamaduni huu uliokithiri unaligharimu Taifa.
“Mali
za umma lazima zitumike kwa shughuli za Serikali na siyo shughuli za
kichama. Hili halina upinzani wala CCM, ni jambo linalotakiwa kupigwa
vita kwa nguvu zote ili rasilimali zetu zitumike ipasavyo,” alisisitiza
kiongozi huyo.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,
Freeman Mbowe alisema limekuwa ni jambo la kawaida kwa CCM kutumia
vyombo vya Dola katika kufanikisha mambo yao na kwamba sababu za kwamba
ndege za Serikali zipo wazi kwa umma ni ‘danganya toto’ ili kufurahisha
wananchi.
“Eti ndege hizo zinaweza kukodiwa na mtu
binafsi au chama, nani kakwambia? Nenda kakodi kama utapata. Ukweli ni
kwamba Magufuli hakuikodi hiyo ndege, kama ni kweli wamekodi watuonyeshe
walilipaje?” alihoji Mbowe na kuongeza.
“Chadema haijawahi kwenda kukodi kwa sababu ina uhakika haitaipata, hasa ikizingatiwa “viwanja tu vya michezo vinavyomilikiwa na CCM havijawahi kutolewa vitumike kwa mikutano ya upinzani tangu mfumo wa vyama vingi uanze zaidi ya miaka 20 iliyopita.”
“Chadema haijawahi kwenda kukodi kwa sababu ina uhakika haitaipata, hasa ikizingatiwa “viwanja tu vya michezo vinavyomilikiwa na CCM havijawahi kutolewa vitumike kwa mikutano ya upinzani tangu mfumo wa vyama vingi uanze zaidi ya miaka 20 iliyopita.”
Mwenyekiti huyo wa Chadema, alisema hata
polisi, mahakama na vyombo vya habari vya Serikali vimekuwa vikitumika
vibaya kuilinda CCM iendelee kukaa madarakani.
Alipoulizwa
juu ya gari la Serikali analotumia kuonekana kwenye mikutano yake ya
kisiasa alijibu: “Nilipopewa gari na Serikali lilikuwa ni kwa matumizi
ya upinzani, mikutano ya kisiasa ninayohudhuria ni sehemu ya kazi za
upinzani… sasa wanaohoji walitegemea nitalitumia gari hilo kwa ajili ya
Serikali? Nenda kawaambie habari ndiyo hiyo na Bunge likivunjwa
nitalirudisha.”
Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii (CCK),
Constatine Akitanda alisema ana shaka kubwa iwapo ndege hiyo ilikodiwa
na CCM na kulipiwa gharama zinazotakiwa.
“Sisi tuna
uhakika gani kuwa CCM walikodi? Hata hizo fedha tukisema twende
tukaangalie je, ni kweli wamelipa au wamechukua tu hiyo ndege?… hata
ukisema tukafanye ‘auditing’ (ukaguzi) hutakuta kitu pale,” alisema
Akitanda.
Ufafanuzi wa wakala
Katika
ufafanuzi wake, Kapteni Mhaiki alisema hakuna haja ya suala hilo
kuchukuliwa kisiasa... “Jukumu la kwanza ni kubeba viongozi wa Serikali
lakini kama kuna muda wa ziada tunawahudumia watu wengine kibiashara na
huwa tunasafirisha hata timu za mpira na wageni kutoka nje ya nchi
wanapotembelea nchini.
“Mtu yeyote anaruhusiwa kuomba kuikodi, atapatiwa ankara yake… hata awe CUF, Chadema au chama chochote kile kama kuna nafasi anapata,” alisema.
“Mtu yeyote anaruhusiwa kuomba kuikodi, atapatiwa ankara yake… hata awe CUF, Chadema au chama chochote kile kama kuna nafasi anapata,” alisema.
Alipoulizwa juu ya tuhuma za
upendeleo kwa chama tawala hivyo kutoleta uwanja sawa wa ushindani,
alijibu: “Upendeleo upi unaozungumza au unautaka? Hata wewe mwandishi
ukitaka tupigie simu ndege ikiwapo utapata.”
TGFA kwa
sasa ina ndege nne ambazo ni Fokker F28 ya mwaka 1978 yenye usajili wa
5H-CCM, Piper PA-31 Navajo (1980, 5H-ILS), Fokker 50 (1992, 5H-TFG) na
Gulfstream 550 ya mwaka 2004 iliyosajiliwa kwa namba 5H-ONE.
Kama mwaka 2010
Sakata
la matumizi ya ndege ya Serikali lilishawahi kujitokeza mwaka 2010
wakati wa kampeni baada ya kumbeba mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama
Salma.
Kitendo hicho kilimfanya aliyekuwa Meneja wa Kampeni kipindi hicho ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuonyesha risiti zilizotumika kulipia huduma za ndege hizo.
Kitendo hicho kilimfanya aliyekuwa Meneja wa Kampeni kipindi hicho ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuonyesha risiti zilizotumika kulipia huduma za ndege hizo.
Mpekuzi blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni