Jumanne, 14 Julai 2015

Emmanuel Mbasha Akutwa na Hatia ya Kesi ya Ubakaji


MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imesema mfanyabiashara na muimbaji wa muziki wa injili Emmanuel Mbasha ana kesi ya kujibu katika shtaka linalomkabili la ubakaji linalomkabili.
 
Katika shtaka hilo Mbasha anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 17 (jina linahifadhiwa) ambaye ni shemeji yake.
 
Mbele ya Hakimu Flora Mjaya, mwendesha Mashtaka Munde Kalombola alidai mahakama imemkuta Mbasha na hatia baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili.
 
Mbasha ambaye ni mume wa muimbaji maarufu wa muziki wa injili Flora Mbasha anadaiwa kumbaka shemeji yake huyo kati ya Mei 23 na 25 mwaka huu eneo la Tabata ambako alikuwa akiishi naye.
 
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mahakamani hapo Septemba 5, 2013 ambapo binti huyo aliieleza Mahakama kuwa alibakwa na shemeji yake (Mbasha) kwa awamu mbili tofauti kabla ya kufanikiwa kukimbia.
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2003 sura ya 20 kifungu cha 186, kifungu kidogo cha tatu, kesi hiyo inasikilizwa na Mahakama ya siri ili kulinda haki ya binti huyo.
 
Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Julai 23, mwaka huu ambapo Mbasha anatakiwa kufika na mawakili wake ili kujitetea dhidi ya shtaka hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa