Kufuatia skendo ya utapeli inayoendelea kumwandama mwimbaji wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando anadaiwa kupigwa pingu mkoani Dodoma, baadaye akasafirishwa hadi Dar kwa msimamizi wa kazi zake, Alex Msama, kwa lengo la kumlipia deni alilokuwa akidaiwa.
Habari kutoka kwa chanzo zimeeleza kwamba, hivi karibuni, Rose
alilipwa Sh. milioni 3 kwa ajili ya shoo huko Makambako mkoani Njombe na
matangazo yakafanyika lakini hakutokea.
Ikadaiwa kuwa, wakati matangazo ya shoo yakiendelea, mtu mwingine
aliyekuwa akimdai Sh. milioni 3.5 (pia alichukua fedha kwa shoo siku za
nyuma) alikwenda Makambako kwa lengo la kumsubiri Rose ili amnase,
lakini hakutokea.
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘unyunyuzi’ kuwa, wawili hao
waliripoti ishu ya Rose, Kituo cha Polisi Makambako ambapo polisi
walifunga safari kumfuata Dodoma.
Sosi huyo alisema kuwa, Rose alikamatwa Juni 27, mwaka huu na
kuswekwa rumande Kituo Kikuu cha Polisi, Dodoma tayari kwa kupelekwa
mahakamani.
Imedaiwa kuwa, kigogo mmoja wa serikali mkoani humo (jina lipo) aliwaambia polisi wampigie simu Msama na kumweleza kisanga hicho ili ikibidi yeye amlipie deni hilo kwa sababu anamsimamia kazi zake.
Imedaiwa kuwa, kigogo mmoja wa serikali mkoani humo (jina lipo) aliwaambia polisi wampigie simu Msama na kumweleza kisanga hicho ili ikibidi yeye amlipie deni hilo kwa sababu anamsimamia kazi zake.
“Msama alikubali kwa sharti kwamba, kwa sababu ana kazi ya kufanya na
Rose hivyo asafirishwe hadi Dar amlimpie, yeye na Rose watakatana
kwenye kazi.
“Rose alisafirishwa Juni 29, mwaka huu akiwa chini ya ulinzi wa
askari wawili. Mmoja wa kike ambaye alilala naye chumba kimoja hotelini.
Kesho yake wakaenda ofisini kwa Msama, Block 41, Kinondoni, akalipa
milioni sita na laki tano keshi,” kilisema chanzo.
Mpekuzi blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni