Mbunge wa Monduli Edward Lowassa pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya muungano wa Tanzania wamechukua fomu za kugombea urais kwa tiketi ya
chama cha Mapinduzi .
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua Fomu mbunge
wa Monduli Edward Lowassa aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha katika dftari la kudumu la wapiga ili waweze kupata haki
yao ya kikatiba ya kupiga kura.
Akijibu moja ya swali lililoulizwa kuhusu mpango kama akishindwa
kuteuliwa kugombea urais Lowassa amesema kamwe hawezi kushindwa katika
kinyang’anyiro hicho cha urais.
Kwa upande wake Makamu wa Rais Dk Mohamed Bilal alisema endapo
atachaguliwa kuwa rais kupitia chama cha Mapinduzi atatekeleza
vipaumbele vifuatavyo;
-Kulinda misingi ya utaifa na kuimarisha umoja na uhuru
-Kuunusuru muungano ambao ni wa kipekee barani Afrika
-Kuwa na Tanzania Shindani
-Kusimamia miiko ya uongozi na utumishi wa umma
-Kuendeleza ushirikiano na mataifa mengine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni