Waziri
Mkuu Wa zamani Edward Lowassa anatarajia kwenda makao makuu ya chama
cha Mapinduzi maarufu kama White House mkoani Dodoma june 3
akisindikizwa na maelfu ya wananchi.
Kwa
mujibu wa Mnyetishaji wetu aliyezungumza na mtandao huu,
amearifu kuwa wakazi wa Manispaa ya Dodoma watakwenda kumpokea Mbunge
wa Monduli Edward katika wilaya ya Manyoni akitokea mkoani
Arusha kwenda mkoani Dodoma kuchukua fomu ya kugombea Urais kwa tiketi
ya chama cha Mapinduzi (CCM).
Aidha,
wagombea wote wanaotaka kuwania urais kupitia chama cha Mapinduzi
wanatakiwa kuchukua fomu ifikapo tarehe 3/6/2015 na kurudisha
2/7/2015. Kutafuta wadhamini mikoani ni 3/6/2015 hadi 2/7/2015.
Kamati
ya usalama na maadili itakutana 8/7/2015 ikifuatiwa na kamati ya
Halmashauri kuu ya Taifa 9/7/2015. Uteuzi wa wagombea urais
utafanyika Zanzibar tarehe 10/7/2015 ukifuatiwa na mkutano mkuu Taifa
wa tarehe 11-12/7/2015.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni