Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuri jana alichukua fomu ya
kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi.
Akizungumza mara baada ya kupokea fomu ya kugombea Urais Magufuri
alisema kwamba hajui kwenye fomu hizo kimeandikwa nini hivyo kuomba
muda zaidi wa kuzisoma na kuahidi kuwa atazungumza na Waandishi wa
Habari muda ukifika.
Katika hatua nyingine Magufuri alisema kwamba moja ya kipaumbele
chake ni kutekeleza ilani ya chama Cha Mapinduzi katika kitabu cha ilani
alichokishika wakati akichukua fomu ya kugombea urais.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni