Jumanne, 30 Juni 2015

KUMEKUCHA MAPEMAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!! POST ZA KIDATO CHA TANO HIZI HAPAAAAAAAAAAAAAAA

TAARIFA KWA UMMA

OWM-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwakujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2015.Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.

Jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana31,700 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 nawavulana 18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansina Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 nawavulana 13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomoya Sanaa na Biashara.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015wataanza muhula wa kwanza tarehe 18 Julai, 2015 na hakutakuwa nafursa ya mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwakuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunziatachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho yakuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosanafasi.

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano naVyuo vya Ufundi mwaka 2015 inapatikana kwenye tovuti ya OWMTAMISEMI
ya www.pmoralg.go.tz

Imetolewa na Katibu Mkuu,

Tangazo




Post:

Uchaguzi Kidato Cha 5::.


Kila la kheri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa