Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya Tatu Fredrick Sumaye pamoja na
Amos Siyatemi jana wamechukua fomu za kugombea urais kwa tiketi ya chama
cha Mapinduzi makao makuu ya CCM Mkoani Dodoma .
Pazia la kuchukulia fomu lilifunguliwa na Amos Siyatemi majira ya nne akifuatiwa na Sumaye majira ya saa tano na nusu.
Akizungumza wakati wa kuchukua fomu Sumaye alisema moja ya
kipaumbele chake ni kupamabana na rushwa, ufisadi na mauaji ya albino
yanayoendelea nchini Tanzania hivisasa.
Kipaumbelea chake kingine ni
kukuza uchumi ili kukabiliana na wimbi la vijana wanao maliza vyuo vikuu
pamoja na vyuo vingine.
Alisisitiza kuwa ataunda kitendo cha kuhujumu uchumi pamoja na kutenga kati ya wafanya biashara na watendaji wa serikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni