Jumatano, 10 Juni 2015

Magufuli Aendelea Kusaka Wadhamini, Agoma Kuzungumza


Waziri wa ujenzi Dkt. John Pombe Magufuri ambaye pia ni miongoni mwa wagombea waliochukua fomu za kuwania mbio za uraisi wa awamu ya tano amesema hawezi kuthubutu kuzungumza chochote mbele ya hadhara ya wananchi katika kipindi hiki kigumu cha kutafuta wadhamini na kwamba kufanya hivyo nikukiuka maadili ya chama chake.

Akizungumza mjini Bukoba wakati wa akitoa shukrani zake kwa waliojitokeza kumdhamini, waziri Magufuli amewaambia wadhamini wake mkoani Kagera kwamba hawezi kuongea kitu chochote juu ya nini atawafanyia wananchi endapo atachaguliwa kushika nafasi ya urais wa awamu ya tano na kuongeza kuwa muda wa kufanya hivyo bado haujafika kwa kuwa kampeni hazijaanza, hivyo wanaotoa ahadi wanakiuka kanuni za chama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa