STAA wa Bongo movies, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, ametoa kali kwamba
katika maisha yake ya mapenzi hajawahi kulala na mwanaume kwenye nyumba
za wageni.
Kabula alisema wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi walipotaka kumpeleka
katika nyumba hizo aligoma na badala yake aliwataka wampeleke wanapoishi
kama hataki hapati kitu.
“Siwezi kuficha, ukweli ndio huo kama huamini basi, mwanaume akinitaka
huwa ananipeleka kwake sio gesti kama hataki aniache tu, naendeleza
rekodi yangu ya kutolala na wanaume gesti,’’ alieleza Kabula.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni