Alhamisi, 23 Julai 2015

Mbowe Asema UKAWA Wana Mgombea Makini.......Asema Atajulikana hivi punde



MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe amesema pamoja na changamoto wanazokumbana nazo katika Ukawa, lakini wanajitahidi kumpata mgombea mmoja.

Jumatatu, 20 Julai 2015

CUF Yasema CCM Ilimuonea Edward Lowassa.......Yasema Ipo Tayari Kumpokea Kwa Kuwa Ni Mtu Safi, Asiye Na Doa lolote


Chama  cha Wananchi (CUF), kimeibuka na kumtetea aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (pichani juu), kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilimuonea kwa kukata jina katika ngazi ya Kamati ya Maadili na kushindwa kulifikisha  Kamati Kuu ya CCM (CC).

Upinzani waja juu Magufuli kutumia ndege ya Serikali


Wanasiasa wa upinzani nchini wamepinga kitendo cha mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kutumia ndege ya Serikali kwenye shughuli za kichama za kujitambulisha wakisema hatua hiyo ni matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa.

Chadema yatangaza ratiba kura ya maoni.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza ratiba ya kuanza kura ya maoni ndani ya chama hicho kuwa itaanza leo (Julai 20) na kumalizika Julai 25 mwaka huu.

Jumatano, 15 Julai 2015

MATOKEO UALIMU 2015

Tafadhali bofya kwenye jina la mtihani husika kuangalia

DSEE
DTE
GATCE
GATSCCE

MPYAAAAAAAA KABISAAAAAAAAAAA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA HAYA HAPAAAAAAAAA

Matokeo ya Kidato cha Sita yametangazwa mtandaoni rasmi na Baraza la Mitihani nchini almaarufu kama NECTA. Kuyaona matokeo hayo ingia hapa:NECTA | View News

http://necta.go.tz/matokeo/2015/Alevel.htm


Name:  NECTA 6.png
Views: 79
Size:  62.5 KB

MWANDISHI WA HABARI ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO JIPYA LA USHETU KWA TIKETI YA CHADEMA


SHINYANGA
MWANDISHI wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” ameamua kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo la jipya la Ushetu katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyaga,kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.

MGOMBEA WA UKAWA KUTANGAZWA NDANI YA SIKU SABA


Mgombea urais ndani ya UKAWA kuja kutangazwa kwa shamrashamra ni ndani ya siku saba.

Jumanne, 14 Julai 2015

Emmanuel Mbasha Akutwa na Hatia ya Kesi ya Ubakaji


MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imesema mfanyabiashara na muimbaji wa muziki wa injili Emmanuel Mbasha ana kesi ya kujibu katika shtaka linalomkabili la ubakaji linalomkabili.

Tukio la Kituo cha Polisi Kutekwa: Viongozi Wa Dini Wacharuka.......Wamtaka Rais Kikwete Afanye Mabadiliko ya Jeshi la Polisi


VIONGOZI mbalimbali wa dini nchini wameandaa maandamano  kwa lengo la kumuona Rais jakaya kikwete ili kumuomba alifanyie mabadiliko makubwa Jeshi Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Azungumzia Tukio La Majambazi Kuvamia Kituo Cha Polisi Jana.......Asema Waliouawa ni Polisi 4 na Wananchi 3

Mpekuzi blog

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam, kutokana na Askari wa Jeshi la Polisi  na raia wa eneo hilo kuuwawa na majambazi waliovamia katika kituo hicho usiku wa kuamkia leo

Majambazi Yalitikisa Tena Jiji la Dar es Salaam


Mmoja wa watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi akiwa mikononi mwa polisi baada ya kutiwa mbaroni Mnara wa Saa maeneo ya Stesheni jijini Dar es Salaam leo mchana kwa madai ya kupora kiasi kikubwa cha fedha. Watu hao wanadaiwa kuwa walikuwa wanne.

Jumatatu, 13 Julai 2015

Urais 2015: Magufuli amteua makamu wa Rais Mwanamke


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuri mara baada ya kuteuliwa kuipeperusha Bendera ya Chama cha Mapinduzi(CCM) katika uchaguzi mkuu ujao amemteua Samia Suluhu Hassan kuwa makamu wake wa Rais endapo atashinda katika uchaguzi mkuu ujao.

URAIS 2015: MEMBE, KIGWANGALLA WAKUBALI YAISHE


Waziri wa Mambo ya nje na  Ushirikiano wa  Kimataifa Mh. Bernard Membe  pamoja na  Mbunge wa Nzega  Dkt. Hamisi Kigwangalla wamekubali kushindwa katika kinyang’iro cha kuomba ridhaa ya kuteuliwa ndani ya chama cha Mapinduzi CCM zoezi lililohitimishwa leo.

Jumanne, 7 Julai 2015

Mambo Yameanza Kupendeza Dodoma.......Tazama Picha 11 za Ukumbi Mpya Wa CCM Utakaotumika Kumtangaza Mgombea Atakayeteuliwa na CCM


Muonekano wa nje wa Jengo jipya la Ukumbi wa Mikutano wa kisasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Dodoma. 

Achakazwa Sura na Mke Mwenziye


“Dunia imeharibika na binadamu hawana upendo wamegeuka kuwa na tabia kama za wanyama kila kukicha…” hiyo ni kauli yake Rehema Gwaya (41) mkazi wa Barabara ya Sokoine, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Ukatili mkubwa Mtoto atekwa, abakwa hadi kupoteza maisha


Mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina la Ester Banzi, mkazi wa Tabata Msimbazi, jijini Dar es Salaam, ametekwa na kubakwa hadi kupoteza maisha baada ya mtu asiyefahamika kufanya kitendo hicho na kutokomea sehemu isyojulikana.

LIPUMBA: Tutaitisha Maandamano Mikoa Yote Yenye GESI


Chama cha Wananchi (CUF), kimesema kitaitisha maandamano kwenye mikoa yenye gesi ili kulishinikiza Bunge kupinga muswada wa mafuta na gesi uliopitishwa juzi.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza Ashitakiwa Mahakamani Jijini Arusha Kwa Kukiuka Katiba Ya Nchi Hiyo


Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameshitakiwa katika Mahakama ya Afrika Mashariki iliyopo jijini Arusha kutokana na hatua yake inayotajwa kukiuka Katiba ya nchi hiyo kwa kuwania kipindi cha tatu cha Urais.

Lowassa Asukiwa Zengwe Ili Jina Lake LIKATWE


Wakati joto la uchujaji wa majina ya wagombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) likizidi kuongezeka, taarifa zimezidi kuzagaa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kwamba, mikakati ya kumuondoa Edward Lowassa kwenye orodha ya watia nia nayo imezidi kupamba moto.

Jumatatu, 6 Julai 2015

Dr Shein Apitishwa Kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia CCM.


Kamati kuu maalum ya chama cha mapinduzi Zanzibar kwa kauli moja imempitisha Dr Ali Mohamed Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi.

Utafiti Urais 2015: Lowassa Aongoza Mbio za Urais.........Dr Slaa Ashika Nafasi ya Pili


Zikiwa zimebakia siku sita kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumpata mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu,

Rose Mhando Apigwa Pingu Dodoma......Asafirishwa Kwenda Dar


Kufuatia skendo ya utapeli inayoendelea kumwandama mwimbaji wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando anadaiwa kupigwa pingu mkoani Dodoma, baadaye akasafirishwa hadi Dar kwa msimamizi wa kazi zake, Alex Msama, kwa lengo la kumlipia deni alilokuwa akidaiwa.

Basil PesaMbili Mramba na Daniel Yona Wahukumia Kifungo cha Miaka Mitatu na Faini ya Milioni 5 Kila mmoja


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, imewahukumu kifungo cha miaka mitatu jela aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Bazil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona baada ya kuwatia hatiani kwa makosa mawili.

UKAWA Wajitoa Rasmi Bungeni....Waondoka Mjini Dodoma


UMOJA wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA leo umetangaza rasmi kususia vikao vya bunge vilivyobaki kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni za bunge. 

Jumapili, 5 Julai 2015

Mlipuko wawaua watu 11 Baghdad

 
Iraq
Mashambulizi ya mabomu yamewaua takriban watu 11 katika wilaya zenye washia wengi kwenye mji mkuu wa Iraq Baghdad.
Magari yaliyokuwa yametegwa mabomu yalilipuka wakati watu walipokuwa wakifungua siku ya mwezi mtukufu wa ramadhan.
Haijabainika yule alitekeleza shambulizi hilo lakini utawala nchini Iraq unawalaumu wanamgambo wa Islamic state kwa mashambulizi yote ya karibu kila siku mjini Baghdad.

Wagiriki waamua kuhusu madeni yao


Ugiriki
Mamilioni wa raia nchini Ugiriki wanapiga kura ya maamuzi kuhusu iwapo watakubali ama kukataa masharti yaliowekwa na wakopeshaji ili kulipa deni wanalodaiwa.
Akipiga kura,waziri mkuu Alexis Tsipras amesema kuwa hakuna anayeweza kupuuza uamuzi wa raia.

Wikileaks:Marekani iliichunguza Brazil


Dilma Rousseff
Mtandao wa Wikileaks umesema kuwa una ushahidi kwamba baadhi ya maafisa wakuu wa taifa la Brazil walipelelezwa mara kadhaa na idara ya ujasusi nchini Marekani NSA.
Habari hizo zinasema kuwa Idara hiyo hususan ilipeleleza uchumi wa taifa hilo.
Wikileaks ilichapisha orodha ya nambari 29 za simu za raia wa Brazil waliopo katika sekta za benki,fedha na uchumi.

Majeshi ya muungano yashambulia IS Syria



 
Ndege za majeshi ya muungano
Ushirikiano unaoongozwa na Marekani, unasema kuwa umefanya mashambulio makubwa ya ndege dhidi ya shina la wapiganaji wa Islamic State, katika mji wa Raqqa, wa Syria.

Alhamisi, 2 Julai 2015

Polisi Yanasa Mtambo Wa Kutengeneza Bunduki


POLISI mkoani Rukwa imewakamata watuhumiwa 19 na silaha za aina mbalimbali zikiwemo bunduki 30, risasi 231 pamoja na mtambo wa kutengeneza bunduki za kienyeji.

Mwalimu Ahukumiwa Kifungo Cha Maisha Jela Kwa Kumnajisi Mkjuu Wake


MWALIMU mstaafu, Rashid Mbogo (65) amehukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi baada ya kupatikana hatia ya kumnajisi mjukuu wake wa kike mwenye umri wa miaka mitano.

Urais 2015: UKAWA Waahidi Neema Kwa Wachimbaji


SERIKALI itakayoundwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) imeahidi kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogowadogo ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo katika shughuli za uchimbaji wa madini huku ikihakikisha kuwa kampuni kubwa za uwekezaji zikilipa kodi stahiki ya Serikali.

Wanne Wahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa Baada Ya Kukutwa Na Hatia Ya Kumuua Albino


MKAZI wa Kiwira, wilayani Rungwe, Hakimu Mwakalinga ambaye aliwahi kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kukutwa na hatia ya kumuua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Rungwe, John Mwakenja, amehukumiwa adhabu hiyo kwa mara nyingine baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mlemavu wa ngozi (albino).

Lowassa: "Nimechoka Kuitwa Fisadi .......Mwenye Ushahidi wa Rushwa dhidi Yangu Ajitokeze Ili Aeleze nilitoa lini, wapi na kwa nani."


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana aliwataka wanaomhusisha na ufisadi kuacha mara moja kwa sababu hakuna hata chembe ya ukweli katika tuhuma hizo.

CHADEMA Yaibwaga CCM Mahakamani........Matokeo ya Uchaguzi Wenyeviti 16 Yatenguliwa


Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara imezidi kupata pigo baada ya Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji 16 vya mji mdogo wa Mirerani, kwa maelezo kuwa ulikiuka sheria na utaratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. 

Jumla ya Mara Iliyotazamwa