Askari
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha 27 Makoko kilichopo
Musoma, Praiveti Wilfred Koko amekutwa ameuawa na kuondolewa sehemu ya
viungo vya mwili katika eneo la kikosi hicho.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani Mara ilisema askari
huyo MT-78227, aliokotwa katika eneo la jeshi Januari 30, mwaka huu saa
sita mchana mwili wake ukiwa hauna baadhi ya viungo ukiwemo mguu wa
kulia, viganja vya mikono yote na sehemu za siri.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ernest Kimola, alisema upande
wa mguu wa kushoto wa marehemu ulikutwa na jeraha lililokatwa na kitu
chenye ncha kali hali inayoonyesha huenda askari huyo aliuawa na kutupwa
kwenye eneo hilo.
Alisema huenda viungo vya askari huyo ambavyo havikukutwa vilikuwa
vimeliwa na wanyama baada ya mwili huo kuonekana kukaa muda mrefu,
kuanza kuharibika na kuingiliwa na wadudu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni