Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (wa pili
kushoto) akizungumza katika mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na
ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la
kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na
Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo
hicho,jijini Dar es salaam.Ujumbe huo unaongozwa na Waziri wa Masuala ya
Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig (wa pili
kulia). Picha zote na Othman Michuzi.
Mratibu wa Uwekezaji wa Kimataifa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC),Zacharia Kingu akifafanua jambo wakati akiwasilisha taarifa ya
uwekezaji katika maeneo mbali mbali nchini wakati wa mkutano maalum kati
ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini
Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara
kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa
Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es salaam.
Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani pamoja uongozi wa
TIC ukifatikia kwa makini taarifa ya uwekezaji iliyokuwa ikitolewa na
Mratibu wa Uwekezaji wa Kimataifa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC),Zacharia Kingu (kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet
Kairuki (katikati) akitoa ufafanuzi wa maswala mbali mbali ya uwekezaji
kwa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani waliotembelea
kituo hicho jana jioni,jijini Dar es salaam.
Kiongozi wa Msafara wa Wafanyabiara hao ambaye ni Waziri wa Masuala
ya Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig
akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC),Juliet Kairuki.
Meneja wa Kitengo cha Uratibu Miradi ya Ubia (Sekta ya Umma na
Binafsi) wa TIC,Said Amir akitoa ufafanuzi juu ya maswala ya ubia katika
miradi,wakati wa mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa
wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na
kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika
jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es
salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirika wa Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC),Revocatus Arbogust akichangia jambo katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet
Kairuki (katikati) akifafanua jambo katika mkutano maalum kati ya
Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini
Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara
kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa
Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es salaam.
Kiongozi wa Msafara wa Wafanyabiara hao ambaye ni Waziri wa Masuala
ya Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig
akizungumza na mmoja wa wafanyabiashara aliofatana nao.
Sehemu ya Wafanyabiashara hao wakifatilia kwa makini taarifa ya uwekezaji.
Sehemu ya Ujumbe wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ukifatilia kwa makini mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet
Kairuki (wa pili kushoto) akiongea na ujumbe huo wakati akiwaonyesha
moja ya Jengo lilalotumiwa Kituo hicho lililojengwa na Wajerumani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni