Ijumaa, 6 Februari 2015

TANZANIA KUBADILISHANA WAFUNGWA NA NCHI ZA THAILAND NA MAURITIUS


indexNa Lorietha Laurence-Maelezo,Dodoma
SERIKALI ya Tanzania imeingia mkataba wa kubadilishana wafungwa kwa nchi za Thailand na Mauritius ambapo hadi sasa Tanzania imeweza kupokea wafungwa kumi kutoka nchi hizo kutekeleza mkataba huo.
Hayo yameelezw a na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Pereira Silima alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Ritta Kabati aliyetaka kujua u ni nchi zipi Tanzania imesainiana nazo mkataba wa kubadilishana wafungwa.
Naibu Waziri Silima aliongeza kuwa katika kutekeleza mkataba kati ya wafungwa hao 10, tisa wameshamaliza hukumu za vifungo vyao huku mmoja anategemea kumaliza kutumikia kifungo mwaka 2021.

“Mpaka sasa Serikali yetu imeweza kuhudumia wafungu kumi kutoka nchi hizo mbili ambapo mwanamke mmoja na wanaume tisa” alisema Silima
Aidha aliongeza kuwa kupitia diplomasia ya mahusiano baina ya nchi na nchi, Serikali inaweza kuingia mkataba na nchi nyingine tatu ambazo ni Kenya, China na India ambako wananchi wake waamekuwa wakitumikia vifungo mbalimbali.
Vilevile alitoa wito kwa Watanzania wanaosafiri katika nchi mbalimbali kuzijua sheria na taratibu za nchi hizo ili kutoingia katika matatizo pamoja na wajiupushe na biashara haramu ikiwemo ya dawa za kulevya.
Pia kwa upande wa wale wanaotumikia vifungo katika nchi ambazo Tanzania haina mkataba nao wa kubadilishana wafungwa, waweze kuwasiliana na balozi za Tanzania ili kupata msaada wa kisheria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa