Jumatano, 4 Februari 2015

Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt atembelea Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha Polisi Temeke leo


Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt akisalimiana na maofisa wa Jeshi la Polisi wakati alipotembelea Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha Polisi Cha Temeke leo.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, DCP Adolphina Chialo akitoa ripoti ya dawati la jinsia na watoto tokea kuanzishwa kwake wakati mke wa rais wa Ujerumani Bi Daniella Schadt alipotembelea dawati la jinsia na watoto katika Kituo cha Polisi cha Chang'ombe kilichopo Temeke.

Baadhi ya wafanyakazi wa UNICEF, Viongozi wa Jeshi la Polisi pamoja na wadau wakisikiliza kwa makini ripoti fupi iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Jeshi la Polisi Nchini, DCP Adolphina Chialo (hayupo pichani).

Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt akipelekwa katika ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto iliyopo katika kituo cha Polisi Chang'ombe Temeke wakati alipotembelea kituo hiko kuona jinsi Dawati hilo linavyofanya kazi.


Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt akibadilishana mawazo na ripota vijana wa UN kabla ya kufanya nao mahojiano mara baada ya kumaliza kuongea na viongozi wa dawati la jinsia na watoto katika Kituo cha Polisi Temeke.


Ripota vijana wa UN wakifanya mahojiano na Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt mara baada ya kumaliza kutembelea ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha Polisi Temeke.

Akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Jeshi la Polisi, ripota vijana wa UN.Picha na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa