Ikiwa
imepita wiki moja tu tangu asajiliwe na klabu ya Italia ya Sampdoria,
mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto’o ameripotiwa
kuwa kwenye utata wa kutaka kuihama klabu hiyo baada ya kutoelewana na
kocha wake.
Kilichotokea
ni kwamba Eto’o aliingia kwenye matatizo na kocha Sinisa Mihaijlovic
baada ya kocha huyo kumtaka afanye mazoezi ya ziada baada ya mchezo
ambao Sampdoria ilifungwa 5-1 na timu ya Torino katika muendelezo wa
ligi ya Italia maarufu kama Serie A.
Kwenye
hiyo mechi Eto’o aliichezea klabu yake mpya kwa mara ya kwanza baada ya
kuingia akitokea benchi kwenye dakika ya 71 japo uwepo wake haukuweza
kuiokoa timu yake na kipigo ilichokipata toka kwa Torino .Eto’o na kocha
wake walifanya kikao cha dharura kuzungumzia kilichotokea baada ya
mshambuliaji huyo kuamua kuondoka na kwenda Milan ambako familia yake
ipo.
Inasemekana
kuwa uhusiano kati ya Eto’o na kocha wake umefikia hatua mbaya kiasi
cha klabu hiyo kuwa na wazo la kuvunja mkataba wake wamiaka miwili baada
ya kusaini ndani ya wiki moja tu akitokea Everton.
Viongozi
wa klabu hiyo ya Sampdoria wamekataa kuzungumzia tukio hilo wakisisitiza
kuwa eto’o alikosa mazoezi kwa sababu zake binafasi lakini kocha
anasema ‘Club ndio itajua nini cha kufanya ila kwangu mimi mchezaji
anapofanya kitu kama hiki ni amenikosea heshima na kunidharau mimi na
wafanyakazi wengine, aliondoka mazoezini bila kuniaga au kuomba ruhusa
na hakurudi, sijamuona kuanzia asubuhi na sijaongea nae‘
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni