Mwanamuziki nyota wa miondoko ya Pop ulimwenguni Beyonce
amekuja na biashara mpya inayohusisha chakula ambacho kinashauriwa na madaktari
.
Beyonce ameungana na daktari mmoja anayefahamika kama Marco
Borges ambaye ni mwanasaikolojia wa mazoezi na wawili hawa wamekuja na mpango
wa kufanya biashara ya kupelekea watu vyakula vya mboga ambavyo vinashauriwa na
madaktari
Aina ya chakula atakayouza beyonce itakwenda sambamba na
mpangilio maalum wa kula unaomsaidia mtu kupungua uzito na kubakia katika uzito
wa kawaida unaoshauriwa kiafya huku ukiwa na msaada mkubwa sana kwa watu wenye
matatizo ya uzito .
Biashara hii imetokana na diet ambayo Jay na Beyonce
waliifanya kwa muda wa siku 22 ambapo walikuwa wanakula vyakula vya mboga
pekee.
Beyonce aliamua kuja na wazo hili la biashara baada ya
kufuata mpangilio wa kula wa siku 22 ambao
alifuata akiwa na mumewe Jay Z
mpango ambao unasaidia kupungua uzito na kurutubisha mwili .
Jay Z alizungumzia mpangilio mpya wa chakula ambao yeye na
mkewe wataufuata siku moja kabla ya siku yake ya kuzaliwa ambapo aliandika
kwenye mtandao wa Life and Times kuwa siku moja kabla ya kufikia siku yake ya
kuzaliwa akiwa anatimiza miaka 44 ataanza mpangilio mpya wa chakula ambao
utahusisha vyakula vya mboga pekee.
Hata hivyo bado haijafahamika lini biashara hii ya chakula
ya Beyonce na Marco Borges itaingia sokoni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni