Jumatano, 4 Februari 2015

MSIBA: MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA CCM NEC KWA WILAYA YA LUDEWA ELIZABETH AUGUSTINO HAULE AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 5/02/2015 KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA LUDEWA


 Elizabeth Augustino Haule enzi za uhai wake akiwa katika majukumu ya chama cha mapinduzi wilayani Ludewa.






Katikati mwenye kilemba ni Aliyekuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya ccm taifa(MNEC) Bi.Elizabeth Augustino Haule  kushoto ni Mwenyekiti  wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba kutoka kulia ni mbunge wa jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe.

Aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya ccm Taifa(NEC) wilaya ya Ludewa Bi.Elizabeth Augustino Haule amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 5 Februal 2015 katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa alikokuwa amelazwa tarehe 4 Februal 2015.

Enzi za uhai wake aliweza kuwa muhimili mkubwa kwa vijana ambapo amewahi kuwa katibu wa kikundi cha sanaa cha WUSHU group na baadae kuwa katibu wa IVA YOUTH GROUP na hatimaye kuwa mjumbe wa NEC hivyo mpaka mauti yanamfika amekuwa akitumikia ukatibu wa Iva youth group na Mjumbe wa NEC.

Marehemu Elizabeth alilazwa jana katika hospitali ya wilaya ya Ludewa majira ya saa 5 asubuhi akisumbuliwa na maradhi ya moyo ambayo yamesababisha kuchukua uhai wake.

Aidha Mbunge wa Jimbo la Ludewa kwa chama cha mapinduzi Mh.Deo Filikunjombe ameshtushwa na taarifa hiyo hivyo amewataka wanaccm wilaya ya Ludewa kuwa watulivu kwa kipindi hiki wakati taratibu  nyingine kutoka kwa viongozi wa chama zinafanyika.

Endelea kutembelea mhimbilikwetu.blogspot.com kwa habari zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa