Mwenyekiti wa profesa CUF IBRAHIM LIPUMBA akiwasili katika mkutano huo
Kwa
mara ya Kwanza tangu kutokea kwa vurugu za kisiasa ambazo zilisababisha
mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF profesa IBRAHIM LIPUMBA kupigwa na
kukamatwa na jeshi la polisi na hatimaye kupelekwa mahakamani
mwenyekiti huyo amejitokeza leo jumapili mbele ya wanahabari na kueleza
hali halisi ya tukio hilo huku akieleza adhma yake ya kutaka kumuona
rais kikwete kumueleza matatizo ambayo polisi wa Tanzania wanayo ambayo
yanapaswa kuzibitiwa mara moja.
Akizungumza
kwa uchungu mkubwa LIPUMBA amesema kuwa kilichotokea juzi huko mbagala
ni ishara tosha kuwa Tanzania hakuna amani na democrasia ya kweli kwani
kuzuia maandamanao ambayo kila mwaka huwa yanafanyika kwa amani na
utulivu ni kuwanyima haki watanzania ya kuwakumbuka ndugu zao
waliofariki katika vurugu za Zanzibar.
Amesema
kuwa kitendo walichokifanya polisi kimewasikitisha sana wao kama
wapenda amani na haki kwani polisi hao walikuwa na taarifa tangu tarehe
22 mwezi wa kwanza ila wao wakaja kupiga marufuku maandamano hayo terehe
26 jioni jambo ambalo ni kinyume na utaratibu kwani hawakuwa na muda wa
kuwaambia wanachama wao kuwa maandamano hayo yamepigwa marufuku.
“sasa
nafanya utaratibu wa kistaarabu kabisa wa kwenda kuonana na rais
kikwete na lengo langu ni moja tu la kutaka kumueleza uhalisia wa jeshi
la polisi na vitendo vibaya wanavyovifanya kwani tukiendelea kufumbia
macho matukio kama haya mwisho wa siku tutajikuta mahali pabaya sana
sisi kama nchi hivyo nataka kumueleza kuwa tusiruhusu hali hiyo
itokee.”amesema lipumba.
Aidha
akizungumzia kauli ya serikali iliyotolewa bungeni na waziri wa mambo
ya ndani mh MATHIAS CHIKAWE kuwa CUF walikaidi maagizo ya polisi ya
kusitisha maandamano na ilikuwa ni njia ya kujitafutia umaarufu wa
kisiasa amesema kuwa ni kauli za kutunga na uzushi mkubwa na kauli hizo
zimeonyesha ni jinsi gani serikali imedhamiria kuwapiga wananchi kisawa
sawa katika matukio kama hayo.
Mnamo
tarehe 27 mwezi wa kwanza CUF walikuwa wafanye maandanano ya amani
kuwakumbuka wanachama wenzao waliouawa huko zanzibari lakini maandamano
hayo yaliishia mikononi mwa jeshi la polisi huko mbagala.
Aidha
amewashukuru sana watanzania hususani vyombo vya habari kwa kuonyesha
ushirikiano mkubwa katika sakata hilo na kuuweka ukweli wa jambo hilo
wazi ambapo kila mtanzania ameweza kufahamu ni nini kimetokea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni