Baadhi
ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyoendeshwa na kampuni ya NFT
Consult kwa maofisa rasilimali watu na watoa mafunzo kutoka makampuni
mbalimbali nchini wakifanya usajili kabla ya kuanza kwa warsha hiyo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
MOJA
ya makampuni makubwa yanayoshughulika na ushauri wa jinsi ya kuongeza
ufanisi katika maeneo ya kazi, NFT Consult wameendesha kongamano kubwa
la kutambua haja ya mahitaji ya wadau mbalimbali wa maendeleo hapa
nchini.
Kampuni
hiyo ya kimataifa ambayo imeingia nchini mwaka 2010 ikiwa na matawi
Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini imesema
kongamano hilo limelenga kuonesha uwezo wao katika kubadili mifumo ya
utendaji kazi.
Ofisa
Mtendaji wa kampuni hiyo, Badru Ntege amesema kwamba wamekuwa
wakiendesha mafunzo mbalimbali yenye kueleza thamani ya mfanyakazi na
mdau wowote ambapo uthamini wa wadau ndio unaotoa mwanya wa mabadiliko
chanya yanayotakiwa
“Mafanikio
ya eneo lolote lile linatokana na wadau kusikiliza wenzao na kisha
kufanyia kazi kauli za upande wa pili.” Alisema Ntege.
Timu
ya NFT Consult ikijitambulisha kwa washiriki kabla ya kuanza warsha
hiyo. Kutoka kushoto ni Inside Business Partner wa NFT Consult, Aisu
Mori, Client Partner wa NFT Consult, Immaculate Mwaluko, Ofisa Mtendaji
mkuu wa kampuni ya NFT Consult, Badru Ntege, Meneja biashara mkazi wa
NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan Ajilong na Client Partner wa
NFT Consult, Sophia Shuma.
Alisema
katika mafunzo ya kuthamini ,kanuni kubwa inayotumika ni kujipanga
katika nafasi husika na kutumia changamoto kama fursa za kubadili
mazingira ya kazi na kazi yenyewe ili kupata matokeo yanayotakiwa.
Alisema
kwamba changamoto zinazotolewa na wadau katika kubadilisha mazingira
yao ndio zinatumiwa na kampuni hiyo katika kuhakikisha makampuni na
taasisi zinazotoa huduma zinazokidhi haja kwa muda unaotakiwa katika
mazingira yanayobadilika kwa kasi.
Naye
Meneja biashara mkazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan
Ajilong akizungumzia shughuli wanazofanya alisema kwamba lengo kubwa ya
warsha ya jana ni kuwaeleza wadau nini wanachoweza kuwapa ili wabadili
mazingira yao ya kazi.
Pichani
juu na chini ni Ofisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya NFT Consult, Badru
Ntege akitoa mada kuhusu mifumo saba ya kitabia katika utendaji wa kazi
kwa maofisa rasilimali watu na watoa mafunzo kutoka makampuni mbalimbali
nchini kwenye warsha ya siku moja iliyoratibiwa na kampuni ya JB’s PR
and Events.
Alisema
watu wengi wamechoshwa na mazingira yale yale na kukata tama lakini
kupitia mafunzo yao wamekuwa wakihakikisha kwamba wadau wanapata msukumo
mpya wa kufanyakazi na kupata matokeo chanya kwa kasi.
Alisema
kwamba tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo imefanikiwa kubadili wadau wao
na kuanza kutambua kuthamini watu, kuwasikiliza na kujadiliana nao ili
kupata matokeo yanayotakiwa.
Alisema kwa sasa NFT Consult imepata uzoefu na kufanyakazi katika nchi 6 za kusini mwa jangwa la sahara.
Nchi hizo ni Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
Amesema mabadiliko makubwa katika namna ya kusimamia shughuli kunawezesha mabadiliko ya utendaji na kuleta ufanisi.
Alisema
kazi ya taasisi hiyo pamoja na kusaidia uwapo wa menejimenti na
rasilimali watu zenye uhakika pia husaidia kupatikana kwa kada
inayotakiwa kwa taasisi mbalimbali wakiombwa kufanya hivyo.
Nao
washiriki kutoka TGNP waliohojiwa wakati wa mafunzo hayo walisema ipo
haja kampuni hiyo ikaongea na watendaji wa serikali ili wakapatiwa
mafunzo yatayogeuza changamoto kuwa fursa za kuleta tija katika
uendeshaji wa serikali.
Washiriki
wakijaza chemsha bongo wakati warsha hiyo ya siku moja kwa maofisa
rasilimali watu na watoa mafunzo kutoka makampuni mbalimbali nchini.
“Mafunzo
haya yanawezesha kutambua ubora wa kuthamini na kuhakikisha unasikiliza
kila mtu kwa ajili ya maendeleo, na changamoto za serikali mafunzo haya
yanafaa sana kwao” alisema Shakila Maimana.Alisema anaamini mafunzo hayo yanaweza kugeuza changamoto kuwa fursa za maendeleo.
Naye Diana Sembende alisema kwamba mafunzo hayo yamembadilisha na anaamini kwamba serikalini watumishi wanayahitaji sana.
Kwa matukio zaidi ingia humu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni