Uzalendo wa nchi haupaswi kutawaliwa na itikadi wala ushabiki wa kundi moja dhidi ya kundi jingine la wananchi.
Kilichomuhimu katika uzalendo wa kweli kwa nchi ni upendo wa kilichobora katika kuijenga na kuiimarisha nchi...
Mwaka huu nchi yetu inafanya uchaguzi mkuu kwa ajili ya kupata viongozi wapya wa awamu ya tano tangu ianze kujitawala.
Pamoja na uchaguzi huo kuhusisha wabunge na madiwani, anayelengwa zaidi ni kiongozi mkuu wa nchi, Rais.Huyo ndiye niliyedhamilia kumjadili hapa.
Kwa vile watanzania kiitikadi tumegawanyika katika vyama vingi vya siasa,ni lazima anayefaa kuwa kiongozi wetu mkuu atoke kwenye chama kimojawapo, au pengine hata bila chama kulingana na mfumo utakaokubalika kuendesha uchaguzi huo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Lakini kwa vile watanzania tuko wengi, zaidi ya watu milioni 45,kitu ambacho ni wazi kinaleta ugumu wa kutambuana harakaharaka na kumjua ni yupi anayefaa kuwa kiongozi wetu mkuu kati yetu, inatuwia rahisi kumwangalia mtu huyo kati ya wale walioonyesha nia ya kuitaka nafasi hiyo.
Mpaka sasa walioonyesha nia au kutangaza nia ya wazi ya kuutaka ukuu wa nchi yetu ni makada wa chama tawala,CCM.
Kwa maana hiyo nisieleweke vibaya kwa kuwaangalia hao walioonyesha nia.Ntakuwa sitendi haki kuwasemea ambao hawajawa tayari kuonysha nia za kutaka kuubeba mzigo huo, urais ni mzigo mzito.
Kati ya makada hao wa CCM walioonyesha nia,tukiziweka itikadi zetu pembeni, tunaweza kumpata aliyebora zaidi ya wengine wote, vigezo vya kumpata viko wazi kama ntakavyoonyesha hapo chini.
Kwanza jambo lililorahisisha kazi ya kumweka wazi na kumtambua aliye bora zaidi ya wengine ni mbinu zinazofanyika za kumshamulia mmoja kati ya wote waliotangaza nia ya kuutaka urais wa nchi yetu.
Kwa maana hiyo wanaofanya mbinu hizo wanatuonyesha ni nani wanayemuogopa zaidi, pengine kwa uwezo alionao uliozidi wengine, na hivyo kutufanya tumtambue anayefaa kuichukua nafasi hiyo kuu katika nchi yetu.Naye si mwingine, bali ni Edward Ngoyai Lowassa.
Hilo linaletwa na ukweli wa asili kwamba kati ya miti yote, mti wenye matunda hupata misukosuko mingi kama kurushiwa mawe kila wakati,kupandwapandwa mara kwa mara, kutikiswatikiswa mara nyingi na kadhalika.
Lakini jingine ni kwamba, kawaida ni vigumu kuujua ubaya au uzuri wa kitu kabla ya kukilinganisha kitu hicho na vingine.
Mfano, wakati Lowassa alipolazimika kujiuzulu uwaziri mkuu, wapo waliolichukulia hilo kwamba ni kuyakubali yaliyotendeka kuwa ni makosa yake.
Lakini baada ya kashfa iliyokubwa zaidi ya mara mbili ya kashfa iliyomuondoa Lowassa kutokea na karibu kwa mtindo uleule, lakini bila kutokea kitu chochote kwa nafasi kama aliyokuwa nayo Lowassa, ndipo imejidhihirisha kuwa alichokifanya Lowassa ni kitendo cha uwajibikaji wa kijasiri.
Hicho ni kitendo kinachodhihirisha ubora wake ambao haukuonekana kwa wakati huo kwa vile haukuwa na mahali pa kuulinganisha wala kuufananisha.
Kitendo cha uwajibikaji wa aina hiyo kiliwahi kuonyeshwa na mzee Ali Hassan Mwinyi wakati huo akiwa waziri wa mambo ya ndani, ambaye baadae alikubaliwa na wananchi kuwa Rais.
Ikumbukwe kwamba kuwa na kiongozi wa nchi asiyekubali kuwajibika ni kitu hatari sana.
Hii ni kwa sababu anaweza kufanya lolote kwa kuwa kimamlaka hakuna wa kumfanya lolote
Lakini tukimpa aliyewahi kuonyesha uwajibikaji walau tunakuwa na imani ya kuepukana na hatari hiyo.Huo ndio ubora mwingine wa Lowaasa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni