Jumatano, 9 Desemba 2015

TAZAMA PICHA ZA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA KUFANYA USAFI LEO KATIKA MKOA WA ARUSHA







Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limefanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Mkoani hapa pamoja na Kusafisha kambi zao kwa lengo la kuadhimisha miaka 54 ya uhuru na kutekeleza agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufanya usafi sikukuu hiyo.Pichani ni askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa wamebeba vifaa vya usafi kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo mbalimbali yanayozunguka kambi ya jeshi hilo-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog


Tunakwenda kufanya usafi....Hapa Kazi tu.....

Rais Wa Zanzibar Dk Shein Ashiriki Shughuli za Usafi Kuadhimisha Siku ya Uhuru.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Zanzibar Khatib Abrahman Khatib wakati alipowasilikati eneo la Malindi Mjini Zanzibar katika zoezi ka Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililoshirikisha Viongozi na Wananchi mbali mbali nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizoa taka katika  zoezi ka Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka 54 ya

Rais Magufuli Awaongoza Watanzania Kufanya Usafi

Rais John Magufuli ameongoza kwa vitendo zoezi la kufanya usafi leo kama alivyoelekeza baada ya kufuta shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Uhuru, Disemba 9.

Rais Magufuli Atoa Namba yake Ya Simu Kwa Wavuvi.....Awaahidi Mambo Matatu.

Rais John Magufuli leo ameungana na wananchi katika kufanya usafi ambapo akiwa katika eneo la Feri jijini Dar es Salaam, ameweza kuzungumza moja kwa moja na wavuvi wadogo.

Picha 3 za Waziri Mkuu Akishirikiana na Wananchi Kufanya Usafi Kariakoo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015. 

Alhamisi, 3 Desemba 2015

Magufuli: Sijachangiwa na Mfanyabiashara Yeyote Kuingia Ikulu.


Rais Dk. John Magufuli, amesema hakuna mfanyabiashara aliyemchangia  kumuwezesha kuingia Ikulu katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, ili aweze kusimamia ipasavyo makusanyo ya kodi kwa faida ya wananchi.

Jumanne, 1 Desemba 2015

Sad News: Basi la Takbir Lagongana na Lori Usiku Huu na Kuua Watu Kadhaa


Habari zilizotufikia usiku huu zinaarifu kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha katika ajali mbaya iliyotokea baada ya basi la abiria la Takbir lenye namba za usajili T 230 BRJ lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana na lori eneo la Shelui, kijiji cha Kizonzo omkoani Singida.

MREMA ASEMA HAJUTII KUMNADI RAIS MAGUFULI


MWENYEKITI wa Taifa wa chama cha siasa cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema amesema hakufanya makosa na wala hajutii kumnadi Rais John Magufuli kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa sababu alitambua Watanzania wamelamba dume la maendeleo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano Ya Disemba 2

Jumanne, 17 Novemba 2015

Breaking News: Job Yustino Ndugai Achaguliwa Kuwa Spika wa Bunge la 11 La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma wamemchagua  mheshimiwa  Job Yustino Ndugai kuwa spika wa bunge la Jamhuri wa muungano wa Tanzania.

Katibu wa Bunge Mh Dkt Thomasi Kashilila Amemtangaza Mh Job ndugai  kuwa Spika wa Bunge la 11 baada ya Kujinyakulia Kura 254 sawa na 70% ya Kura zote zilizopigwa.
Mh Ndugai amewashinda Wagombea wengine kutoka vyama na makundi     Mbalimbali

Kura zilizopigwa-365
Kura zilizoharibika-2
Malisa-0
Medeye-109
Rungwe-0
Almasi-0
Ndugai-254
Sarungi-0
Lymo-0
Kasimiu-0

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA LUDEWA KUPITIA C.C.M DEO NGALAWA AIFUNIKA LUDEWA.

Deo Ngalawa akimkabidhi fomu za ubunge msimamizi wa jimbo la uchaguzi la Ludewa Bw.Wiliam Waziri pembeni ni Mwanasheria wa wilaya ya Ludewa Bw.Chalamila



maandamano ya bodaboda yakiendelea kumuunga mkono Bw.Ngalawa

Jumatano, 2 Septemba 2015

Tundu Lissu: Dr Slaa ni Muongo watanzaia Mpuuzeni.....Kinachomsumbua ni tamaa ya Urais. Tunamtaka Arudishe mali zote za Chama


Katibu Mkuu wa  Chadema, Dk Wilbroad Slaa, jana  alitangaza rasmi kuachana na siasa  baada  ya  kutofautiana  na  chama  chake  katika  kumpokea  Edward  Lowassa  na  hatimaye  kumfanya  mgombea  urais  wa  chama  hicho  chini  ya  mwamvuli  wa  UKAWA.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya leo Jumatano ya Septemba 2


Jumanne, 1 Septemba 2015

LIVE UPDATE Kutoka Serena Hotel Ambako Dr. Slaa Anaongea


1.Napenda  kumshukuru  mwenyezi  mungu  kwa  kutujalia  uzima.

2. Nimeamua  kujitokeza  leo  hii  ili  kukomesha  upotoshaji  na  kuuweka  wazi  ukweli.


3.Sina  tabia  ya  kuyumbishwa  na  ninasimamia  ninachokiamini.

4.Sina  ugomvi  na  kiongozi  yeyote  maana  siasa  sio  uadui.

5. Siasa  inapoongozwa  kwa  misingi  ya  upotoshaji, matokeo  yake  ni  vurugu.

6. Naweka  wazi  kuwa  mimi  sikuwa  likizo  na  hakuna  mtu  yoyote  aliyenipa  likizo.

7.Kilichotokea  ni  kuwa  niliamua  kuachana  na  siasa  tangu  tarehe  28.7.2015  saa  sita  usiku  baada  ya  kutoridhishwa  na  kilichokuwa  kinaendelea  ndani  ya  chama  changu.

Sheria ya Makosa ya Mtandao kuanza kutumika leo.



Serikali imewatoa hofu wananchi kuhusu Sheria ya Makosa ya Mtandao inayoanza kutumika rasmi leo kuwa haijatungwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu, bali kwa maslahi mapana ya taifa na kuleta maendeleo ya nchi, kujenga uchumi imara na kupambana na wahalifu.

Lowassa: Miaka 50 ya Kuteswa na CCM Imetosha......Watanzania Msiogope Kufanya Mabadiliko


Mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amesema mwaka huu ni wa mabadiliko ili kuiokoa nchi na madeni mengi ambayo yanasababisha uchumi kuyumba.

Magufuli Atikisa Songea......Aweka shada la maua kwenye Kaburi la Marehemu Kapteni John Komba


Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea jana ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi mkoani humo.

 Akizungumza katika mkutano huo wakati akiomba kura Dr. John Pombe Magufuli aliwaambia wananchi hao kuwa  anataka kuijenga Tanzania mpya yenye viwanda vikubwa, vya kati na vya chini ili kuboresha uchumi wa nchi  na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania na kuleta mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko.
 
 Alisema pia serikali yake itaongeza kasi ya ujenzi wa barabara , Zahanati na Hospitali , kuongeza mafao ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali ili kuongeza tija ya kazi , wanafunzi kusoma bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne nk.
 
 Alisema ataongeza zaidi  kasi yake katika utendaji  tofauti na alipokuwa  Waziri wa ujenzi kwani hapo awali alikuwa akiagizwa kama waziri na sasa  akichaguliwa na watanzania kuwa rais  yeye ndiye atakayeagiza na ole wake waziri atakayemteua asitekeleze maagizo yake atakiona cha moto.
 
 Dr John Pombe Magufuli pia alitembelea  na kuweka shada la maua  kwenye kaburi la Kada maarufu wa CCM marehemu Kapten John Damiano Komba ambaye alifariki  miezi kadhaa iliyopita jijini Dar es salaam katika hospitali ya jeshi Lugalo na kuzikwa nyumbani kwao huko Lituhi wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma ???????????????????????????????????? Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania

Jumatatu, 31 Agosti 2015

PICHA LOWASSA ALIVYOWASILI MKOANI NJOMBE LEO





Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwasili kwenye viwanja vya Shirika la Nyumba (National Housing) Mjini Njombe tayari kwa kuhutubia Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu, anazoendelea kuzifanya kwa nchi nzima. Picha zote na Othman Michuzi, Njombe.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia

Samwel Sitta Awajibu UKAWA


Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta amesema serikali italifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATC) ili liweze kununua ndege nne na kuanza biashara.

AJALI YATOKEA ENEO LA FOREST MPYA BARABARA KUU KUELEKEA ZAMBIA, LORI LIMEKAA VIBAYA , SIKU YA PILI HAKUNA ANAYE HANGAIKA NALO,NI HATARI

  Lori hilo likiwa eneo la tukio ambapo limepatia ajali na hakuna juhudi za kuliondoa
 
 Hii ni Mida ya Mchana jana bado Lilikuwepo na limekaa vibaya ambapo linaweza sababisha matatizo tena

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI JESHI LA POLISI

TANGAZO KWA UMMA.

JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAITA KWENYE USAILI WAHITIMU WALIOORODHESHWA WA SHAHADA, STASHAHADA NA ASTASHAHADA. USAILI UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 03.09.2015 HADI TAREHE 04.09.2015 KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI HADI SAA KUMI JIONI KATIKA MAENEO YAFUATAYO:-
·         FANI YA UTAWALA, UCHUMI, USIMAMIZI WA SHERIA NA UTEKELEZAJI [BALE], UALIMU, UANDISHI HABARI, UHANDISI MADINI [MINING ENGINEERING], UGAVI, LUGHA, USHAURI NASIHI, KATIBU MUKTASI, LAND SURVEY CATHOGRAPHER NA GEOMATICS WATAFANYA USAILI KATIKA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR ES SALAAM [DPA] KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM.

Polisi Yakamata Majambazi 38 Yakiwa na silaha Nzito pamoja na Milioni 170......Majambazi hayo yanadaiwa na mafunzo ya Kijeshi


Jeshi la Polisi limewakamata watu 38 wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi ambao pia wamepatiwa mafunzo ya kigaidi katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Lindi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Septemba 1


Jumanne, 4 Agosti 2015

YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO MKUU WA CHADEMA ULIOFANYIKA LEO NA KUWAPITISHA MH. LOWASSA KUWA MGOMBEA URAIS WA TANZANI

 Mkutano Mkuu wa CHADEMA ulianza kwa kuimba nyimbo ya taifaShehe Rajabu Katimba akiomba Dua wakati wa mkutano mkuu wa CHADEMA uliofanyika leo 

PICHA: Magufuli Alitikisa Jiji la Dar es Salaam Wakati Akichukua Fomu ya Kugombea Urais


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt  John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan wakionesha fomu zao za kuomba kugombea urais

Waziri mwingine, wabunge 4 waanguka kura za maoni CCM


SIKU mbili baada ya mawaziri watano kushindwa katika kura za maoni ya ubunge ndani ya CCM, waziri mwingine, Gaudentia Kabaka anayeshughulikia Kazi na Ajira, naye amedondoshwa katika jimbo la Tarime Mjini.

Alhamisi, 23 Julai 2015

Mbowe Asema UKAWA Wana Mgombea Makini.......Asema Atajulikana hivi punde



MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe amesema pamoja na changamoto wanazokumbana nazo katika Ukawa, lakini wanajitahidi kumpata mgombea mmoja.

Jumatatu, 20 Julai 2015

CUF Yasema CCM Ilimuonea Edward Lowassa.......Yasema Ipo Tayari Kumpokea Kwa Kuwa Ni Mtu Safi, Asiye Na Doa lolote


Chama  cha Wananchi (CUF), kimeibuka na kumtetea aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (pichani juu), kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilimuonea kwa kukata jina katika ngazi ya Kamati ya Maadili na kushindwa kulifikisha  Kamati Kuu ya CCM (CC).

Upinzani waja juu Magufuli kutumia ndege ya Serikali


Wanasiasa wa upinzani nchini wamepinga kitendo cha mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kutumia ndege ya Serikali kwenye shughuli za kichama za kujitambulisha wakisema hatua hiyo ni matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa.

Chadema yatangaza ratiba kura ya maoni.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza ratiba ya kuanza kura ya maoni ndani ya chama hicho kuwa itaanza leo (Julai 20) na kumalizika Julai 25 mwaka huu.

Jumatano, 15 Julai 2015

MATOKEO UALIMU 2015

Tafadhali bofya kwenye jina la mtihani husika kuangalia

DSEE
DTE
GATCE
GATSCCE

MPYAAAAAAAA KABISAAAAAAAAAAA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA HAYA HAPAAAAAAAAA

Matokeo ya Kidato cha Sita yametangazwa mtandaoni rasmi na Baraza la Mitihani nchini almaarufu kama NECTA. Kuyaona matokeo hayo ingia hapa:NECTA | View News

http://necta.go.tz/matokeo/2015/Alevel.htm


Name:  NECTA 6.png
Views: 79
Size:  62.5 KB

MWANDISHI WA HABARI ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO JIPYA LA USHETU KWA TIKETI YA CHADEMA


SHINYANGA
MWANDISHI wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” ameamua kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo la jipya la Ushetu katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyaga,kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.

MGOMBEA WA UKAWA KUTANGAZWA NDANI YA SIKU SABA


Mgombea urais ndani ya UKAWA kuja kutangazwa kwa shamrashamra ni ndani ya siku saba.

Jumanne, 14 Julai 2015

Emmanuel Mbasha Akutwa na Hatia ya Kesi ya Ubakaji


MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imesema mfanyabiashara na muimbaji wa muziki wa injili Emmanuel Mbasha ana kesi ya kujibu katika shtaka linalomkabili la ubakaji linalomkabili.

Tukio la Kituo cha Polisi Kutekwa: Viongozi Wa Dini Wacharuka.......Wamtaka Rais Kikwete Afanye Mabadiliko ya Jeshi la Polisi


VIONGOZI mbalimbali wa dini nchini wameandaa maandamano  kwa lengo la kumuona Rais jakaya kikwete ili kumuomba alifanyie mabadiliko makubwa Jeshi Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Azungumzia Tukio La Majambazi Kuvamia Kituo Cha Polisi Jana.......Asema Waliouawa ni Polisi 4 na Wananchi 3

Mpekuzi blog

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam, kutokana na Askari wa Jeshi la Polisi  na raia wa eneo hilo kuuwawa na majambazi waliovamia katika kituo hicho usiku wa kuamkia leo

Majambazi Yalitikisa Tena Jiji la Dar es Salaam


Mmoja wa watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi akiwa mikononi mwa polisi baada ya kutiwa mbaroni Mnara wa Saa maeneo ya Stesheni jijini Dar es Salaam leo mchana kwa madai ya kupora kiasi kikubwa cha fedha. Watu hao wanadaiwa kuwa walikuwa wanne.

Jumatatu, 13 Julai 2015

Urais 2015: Magufuli amteua makamu wa Rais Mwanamke


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuri mara baada ya kuteuliwa kuipeperusha Bendera ya Chama cha Mapinduzi(CCM) katika uchaguzi mkuu ujao amemteua Samia Suluhu Hassan kuwa makamu wake wa Rais endapo atashinda katika uchaguzi mkuu ujao.

URAIS 2015: MEMBE, KIGWANGALLA WAKUBALI YAISHE


Waziri wa Mambo ya nje na  Ushirikiano wa  Kimataifa Mh. Bernard Membe  pamoja na  Mbunge wa Nzega  Dkt. Hamisi Kigwangalla wamekubali kushindwa katika kinyang’iro cha kuomba ridhaa ya kuteuliwa ndani ya chama cha Mapinduzi CCM zoezi lililohitimishwa leo.

Jumanne, 7 Julai 2015

Mambo Yameanza Kupendeza Dodoma.......Tazama Picha 11 za Ukumbi Mpya Wa CCM Utakaotumika Kumtangaza Mgombea Atakayeteuliwa na CCM


Muonekano wa nje wa Jengo jipya la Ukumbi wa Mikutano wa kisasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Dodoma. 

Achakazwa Sura na Mke Mwenziye


“Dunia imeharibika na binadamu hawana upendo wamegeuka kuwa na tabia kama za wanyama kila kukicha…” hiyo ni kauli yake Rehema Gwaya (41) mkazi wa Barabara ya Sokoine, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Jumla ya Mara Iliyotazamwa