Watu
saba wamefariki dunia 26 wamejeruhiwa baada ya basi la Msanga Express
likitokea Morogoro kwenda Mahenge kugongana na basi la kampuni ya
Luwinzo lililokuwa likitoa Njombe kwenda jijini Dar es Saalam katika
eneo la hifadhi ya Mikumi barabara ya Morogoro Iringa.Wananchi
walioshuhudia tukio hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi
wa dereva wa basi la Msanga Express alikuwa akijaribu kulipita lori bila
tahadhari na kisha kutoa gari barabarani wakati akikwepa ajali ya uso
kwa uso ambapo aligongwa upande wa kulia.
Inaelezwa
kua watu sita walifariki dunia papo hapo na mwingine amefariki wakati
akiwa njiani kupelekwa hospitalini kupata matibabu.Kamanda
wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema hadi sasa mwili mmoja
tu ndiyo uliotambulika na miili mingine sita bado haijatambulika na
imehifadhiwa katika hospitali ya St Kizito Mikumi.
Amesema madereva wa mabasi yote wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu wakiwa chini ya ulinzi ambapo kufuatia kuongezeka kwa mtukio ya ajali za mfululizo katika hifadhi ya Mikumi jeshi la polisi kwa kushirikiana na hifadhi ya Mikumi waanza kufanya oparesheni maalum kukagua madereva wanoendesha kwendo kasi katika hifadhi.
Katika hospitali ya St. Kizito walikolazwa majeruhi muuguzi wa zamu Josefu Masenga amekiri kupokea majeruhi 26 na kueleza amesema hali za majeruhi wanaendelea na matibabu huku majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa wakieleza jinsi tukio lilivyotokea.
-ITV
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni