WANAFUNZI
97 kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma, Tawi la Mbeya, leo wapo Bungeni
mjini Dodoma kwa ziara ya kimafunzo. Wanafunzi hao wanaosomea fani
mbalimbali zikiwepo utunzaji kumbukumbu na makatibu Muktasi watajifunza
vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujioenea moja kwa moja namna
shughuli za Bunge zinavyofanyika.
Mhadhiri
na Kiongozi wa Chuo hicho, Johnson Mbuluma (kulia) akiwa na wanafunzi
wake wakifuatilia shughuli mbalimbali za Bunge mjini Dodoma hii leo.
Wanafunzi hao wakiwa Bungeni wakifuatilia mijadala hiyo mbalimbali na kipindi cha maswali na majibu.
Umakini ulikuwepo wakati wanafunzi hao wakisikiliza na kutaza Wabunge.
Wanafunzi mbalimbali hutembelea Bungeni kwa ajili ya mafunzo na pia makundi mbalimbali katika Jamii. Father Kidevu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni