Hii ndiyo safu mpya ya uongozi wa chama cha walimu wilaya ya Ludewa
Mhasibu wa Chama cha walimu wilaya ya Ludewa Bw.Mvanginyi
Chama cha
walimu wilaya ya Ludewa (CWT) katika mkoa wa Njombe kimetoa tamko kali dhidi ya
uongozi wa Halmashauri ya wilaya la kupinga kitendo cha walimu kukatwa hela
katika mishahara yao kwaajili ya kulipia kodi za nyumba katika maeneo ya kazi.
Tamko hilo
limetolewa na mwenyekiti mpya wa chama hicho Mwalimu Fikiri Mgina baada ya
kumaliza uchaguzi wa vingozi wa CWT
ngazi ya wilaya ambapo aliitaka Halmashauri kutowatoza kodi walimu katika
nyumba wanazoishi kutokana na walimu kufanya kazi katika mazingira magumu na
kutokuwa na posho za muda waziada.
Mwalimu
Mgina alisema kuwa ifike wakati Serikali itambue mchango wa walimu katika
maendeleo ya Taifa na si kuwakandamiza walimu katika kuwatoza michango
inayowaumiza kwani ingefaa nyumba hizo ambazo hazina hazi ya kuishi walimu ziwe
kama motisha kwa walimu.
“Walimu tuko
tayari kuishi chini ya miti na tukiendelea kufanya kazi kutokana na manyanyaso
tunayoyapata kwani kutulipisha kodi za nyumba katika nyumba mbovu ni sawa na
kutunyanyasa,kuna baadhi ya idara wanapata malipo ya ziada wakati wamuda wa
kazi lakini sisi hatuna hilo hivyo nyumba tunazoishi zingekuwa kama motisha kwa
walimu “,alisema Mwalimu Mgina.
Malalamiko
yao ya walimu juu ya kutozwa kodi za nyumba wilayani Ludewa yamekuwa yakitolewa
mara kwa mara huku uongozi wa Halmashauri umekuwa ukisema unalifanyia kazi ili
kupunguza kero hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni