Kamishna
wa Polisi Elice Mapunda akila kiapo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Ernest Mangu baada ya kupandishwa cheo na Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa
Kamishna wa Polisi. Katikati ni Msemaji wa Jeshi hilo Mrakibu Mwandamizi
wa Polisi Advera Bulimba. Hafla hiyo fupi ilifanyinyika jana Makao
Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).
Kamishna
wa Polisi Diwani Athumani akila kiapo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Ernest Mangu baada ya kupandishwa cheo na Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa
Kamishna wa Polisi. Hafla hiyo fupi ilifanyinyika jana Makao Makuu ya
Polisi jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akimpongeza Kamishna wa Polisi
Elice Mapunda mara baada ya kula kiapo mbele yake kufuatia kupandishwa
cheo na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Naibu
Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi. Hafla hiyo fupi
ilifanyinyika jana Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo
maafisa watatu (3) wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Naibu Kamishina wa
Polisi (DCP) kuwa Kamishina wa Polisi (CP) na maafisa wengine 14 kutoka
cheo cha Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) kuwa Naibu
Kamishina wa Polisi (DCP).
Maofisa
waliopandishwa vyeo kutoka cheo cha Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) kuwa
Kamishina wa Polisi (CP) ni pamoja na Kenneth Kasseke, Elice Mapunda na
Diwani Athumani.
Maofisa
wengine waliopandishwa cheo kutoka Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) kuwa Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) ni pamoja na Godluck
Mongi, Ally Lugendo, Salum Msangi, Faustine Shilogile, Maulid Mabakila,
Albert Nyamhanga, Daniel Nyambabe, Salehe Ambika, Robert Boaz na Gabriel
Semiono. Pia wamo kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo,
kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola, kamanda wa Polisi
mkoa wa Arusha Liberatus Sabas na kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Maria
Nzuki.
Aidha,
mhe. Rais amempandisha Juma Yusuf Msige kutoka cheo cha kamishina
msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi
(SACP).
Kufuatia
kupandishwa vyeo kwa maafisa hao wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini IGP Ernest Mangu katika hafla fupi ya kuwaapisha
makamishina hao wapya, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wa Jeshi la Polisi katika
kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Aidha,
IGP Mangu amewapongeza maofisa wote waliopandishwa vyeo na kuwataka
kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa ili kuwa chachu ya
mabadiliko katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao. IGP Mangu
aliongeza kuwa, cheo ni dhamana na kuwataka kuwa mfano mzuri katika
utekelezaji wa majukumu yao na usimamizi kwa walio chini yao.
Imetolewa na:
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni