Jumanne, 17 Machi 2015

FILIKUNJOMBE AWATAKA WANANCHI WA WILAYA LUDEWA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.


 Filikunjombe akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kujiandikisha na kukabidhiwa kitambulisho, mwenye miwani ni kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Prof.Amone Chaligha


 Filikunjombe akiweka alama za vidole katika mashine ya uandikishaji





Mbunge wa jimbo la Ludewa kupitia chama cha mapinduzi katika mkoa wa Njombe Deo Filikunjombe amewataka wananchi wa wilaya ya Ludewa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambalo limeanza leo tarehe 16/3/2015 ili kuweza kupata fulsa ya kuwachagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika ockoba mwaka huu.
Filikunjombe aliyasema hayo jana katika kituo cha uandikishwaji wapiga kura katika shule ya msingi Ludewa mjini wakati akijiandikisha ikiwa ni siku ya ufunguzi wa undikishwaji ulioanza rasmi wilayani hapa na kuwataka wananchi kuachana na maneno ya kizushi ya baadhi ya wanasiasa wanaowarubuni wananchi kutojiandikisha.

Alisema kuwa kwa wananchi wa Ludewa vitambulisho hivyo vitatumika katika matumizi mbalimbali yakiwemo matumizi ya kusajilia simu na mengineyo hivyo hakuna haja ya kukaa kuwasikiliza wasio na mapenzi mema na nchi yao kwa kuwazuia wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba.
“Mimi kama mbunge wajimbo la Ludewa leo nimejiandikisha na tayari nimesha kipata kitambulisho change cha kupigia kura hivyo nawaomba wananchi wangu kujitokeza wote bila kukosa ili kuweza katika kufanikisha zoezi hili wani kitambuisho cha mpiga kura kitawasaidia kwa mambo mengi,msiwasikilize wazushi nisikilizeni mimi ambaye mliniamini na mkanichagua kuwa mwakirishi wenu”,alisema Filikunjombe.
Alisema kama mtanzania unapaswa kujiandikisha na kutumia haki yako ya kikatiba katika kuipigia kura ya ndiyo katiba mpya inayopendekezwa pia kuchagua viongozi mnaowataka ifikapo oktoba mwaka huu.
Aidha kamishna wa tume ya Taifa ya uchaguzi Prof. Amone Chaligha akijubu swali la waandishi wa habari kuhusiana na kasoro za mashine za BVR alisema awali kulikuwa na kasoro za kutosoma kwa baadhi ya watu lakini wataalamu wa mifumo ya Komputor wameshairekebisha hivi sasa hakuna tatizo tena.
Prof.Chaligha alisema kinachotakiwa ni wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani zoezi hilo wilayani Ludewa litafanyika kwa muda wa siku saba na baada ya hapo zoezi litahamia maeneo mengine hivyo hakuna haja ya kuchelewa kujiandikisha.
Alisema tokea zoezi hilo lianze wilayani hapa hakuna kasoro ambazo zimejitokeza kama ilivyokuwa mji wa Makambako hivyo kila mwananchi anatakiwa kutumia fulsa hii ya kujipatia kitambulisho chake sasa ili kuweza kutumia katika upigaji kura.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa