Stakabadhi ambayo Bw.Ocol Haule alipewa na Chadema wilaya ya Ludewa baada ya kutoa fedha kwaajili ya kukijenga chama
Bw.Ocol Haule aliyesimama mwenye koti jeusi akihesabu bati kwaajili ya kwenda Mkiu
Bw.Ocol Haule akiwa na baadhi ya Makamanda wa Chadema wilaya ya Ludewa wakielekea katika mkutano kata ya Mavanga.
Kamanda wa
chama cha Demokrasia na Maendeleo wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe ametoa
kiasi cha shilingi milioni mbili katika ofisi ya chama hicho wilayani hapa
kwaajili ya kukijenda chama hasa katika kipindi hiki cha kuhamasicha wananchi
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Akitoa fedha
hizo katika ofisi ya Chadema ya wilaya ya Ludewa Kamanda huyo ambaye alijitambulisha
kwa jina la Ocol Adrian Haule alisema malengo makuu ya kutoa fedha hizo ni
katika jitihada zake za kukijenga chama na kuiwezesha ofisi ya wilaya kufika
katika maeneo yasiyofikika na kujaribu kuongea na wananchi kuhusiana na
kujiandikisha katika daftari hilo.
Hata hivyo
aliwataka viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya kufanya kazi kwa uaminifu
mkubwa ili kujenga imani kwa wananchi kwani Chadema imekuwa inakubarika katika
maeneo mengi ya nchi kutokana na uaminifu ikiwa na utendaji kazi usio na mashaka
kwa wananchi.
“Nimeamua
kutoa fedha hizi kama kijana pia kamanda wa chama changu ninachokipenda ili kuijengea
uwezo ofisi yetu ya wilaya ambayo bado haijajiimarisha ipasavyo kutokana na nguvu
ya upinzani kwa wilayani Ludewa hivyo nawasihi makamanda wenzangu kuzitumia
fedha hizi kwa malengo yaliyokusudiwa”,alisema Bw.Haule.
Aidha
Bw.Haule aliweza kutoa msaada wa bati 60 geji 28 katika kijiji cha Mkiu shule
ya msingi Mkiu kata ya Mlangali zenye thamani ya shilingi milioni moja laki
mbili na sitini elfu pia pesa ya usafirishaji wa bati hizo kiasi cha shilingi
laki moja na arobaini kutoka Njombe hadi mkiu.
Kutokana na
shule hiyo ambayo imekuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na nyumba ya mwalimu
alisema kuwa huo ni mchango wake yeye kama mzawa wa wilaya Ludewa hivyo aliamua
kutoa kwa malengo ya kuikuza sekta ya elimu wilayani hapa.
Bw.Haule
ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam katika kitivo cha sayansi
ya jamii aliwataka vijana wa wilaya ya Ludewa kumuunga mkono katika suala zima
la kuiendeleza wilaya ya Ludewa kwani bado iko nyuma kielimu na kimaendeleo hivyo
kila mwanaludewa anapaswa kuchangia maendeleo ya wilaya yake.
Mawasiliano yake
sim no.0758358986 au email ocolhaule@gmail.com.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni